Chama Cha Demokrasia makini chasema tutapata ushindi wa “kisulisuli” katika uchaguzi wa serikali za mitaa

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
1574233408436.png

Chama cha Demokrasia Makini kimesema ili kujihakikishia ushindi wa “Kisulisuli” kwa wagombea wake wote, viongozi wote wa ngazi ya juu ya chama hicho wamegawana kwa kila mmoja kwenda katika mkoa wake na kufanya kampeni kwa kadri wanavyoweza kwa kushirikiana na wagombea pamoja na wanachama waliopo katika mikoa hiyo ili kupata ushindi wa Kisulisuli katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mohammed Abdula wakati akizungumza na waandishi wa hanbari kuhusu maandalaizi ya kampeni hizo kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika ujao katika ofisi za chama hicho zilizopo Mabibo jijini Dar es salaam.

Mohammed Abdula ameitaja mikoa ambayo chama hicho kjimesimamisha wagombea kuwa ni pamoja na Morogoro,Mara, Tabora, Kigoma pamoja na Dar es Salaam na kusisitiza kuwa tayari mipango kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni hizo imeshakamilika kwa asilimia mia moja.

“Tutazindua rasmi kampeni zetu za uchaguzi wa Serikali za mitaa Kilosa katika mkoa wa Morogoro na tutaibuka na ushindi wa’Kisulisuli’ katika maeneo yote ambayo tumesimamisha wagombea wetu” . Amesema Mohamed Abdula.

Abdula amesema kumejitokeza kwa baadhi ya vyama kususia uchaguzi huo, kwa upande wa chama hicho hakina mpango huo zaidi kimeamua kuelekeza nguvu zake kuwapigia kampeni kabambe wagombea wake zaidi ya 80 waliopo nchi nzima ili waweze kibuka na ushindi.

“Kutoshiriki uchaguzi ni kujinyima haki ya kidemokrasia, sisi kama chama makini hatuoni sababu yoyote ya kususia uchaguzi huu zaidi tumeamua kwenda kushiriki kikamilifu na mipango yetu ni kuondoka na ushindi katika maeneo yote ambayo wagombea wetu watasimama” alisema Abdula.

Sio rahisi kwa Usimamizi makini wa Tamisemi Chama chako kushinda mkuu
 
Mbona nasikia Dar es Salaam nzima uchaguzi utafanyika mitaa miwili tu? Au ndo hiyo atakayoshinda huyu jamaa?
 
Mzee kazeeka, miaka 75 sio mchezo. Hata upeo wakutambua vitu, umepunguwa
 
View attachment 1267277

Chama cha Demokrasia Makini kimesema ili kujihakikishia ushindi wa “Kisulisuli” kwa wagombea wake wote, viongozi wote wa ngazi ya juu ya chama hicho wamegawana kwa kila mmoja kwenda katika mkoa wake na kufanya kampeni kwa kadri wanavyoweza kwa kushirikiana na wagombea pamoja na wanachama waliopo katika mikoa hiyo ili kupata ushindi wa Kisulisuli katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mohammed Abdula wakati akizungumza na waandishi wa hanbari kuhusu maandalaizi ya kampeni hizo kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika ujao katika ofisi za chama hicho zilizopo Mabibo jijini Dar es salaam.

Mohammed Abdula ameitaja mikoa ambayo chama hicho kjimesimamisha wagombea kuwa ni pamoja na Morogoro,Mara, Tabora, Kigoma pamoja na Dar es Salaam na kusisitiza kuwa tayari mipango kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni hizo imeshakamilika kwa asilimia mia moja.

“Tutazindua rasmi kampeni zetu za uchaguzi wa Serikali za mitaa Kilosa katika mkoa wa Morogoro na tutaibuka na ushindi wa’Kisulisuli’ katika maeneo yote ambayo tumesimamisha wagombea wetu” . Amesema Mohamed Abdula.

Abdula amesema kumejitokeza kwa baadhi ya vyama kususia uchaguzi huo, kwa upande wa chama hicho hakina mpango huo zaidi kimeamua kuelekeza nguvu zake kuwapigia kampeni kabambe wagombea wake zaidi ya 80 waliopo nchi nzima ili waweze kibuka na ushindi.

“Kutoshiriki uchaguzi ni kujinyima haki ya kidemokrasia, sisi kama chama makini hatuoni sababu yoyote ya kususia uchaguzi huu zaidi tumeamua kwenda kushiriki kikamilifu na mipango yetu ni kuondoka na ushindi katika maeneo yote ambayo wagombea wetu watasimama” alisema Abdula.

Kuna vichaa hii dunia aisee
 
Sio chama pandikizi ili ionekane uchaguzi ulifanyika
 
Kusanifiana huku!. Eti Chasema hahaa kikipeperusha bendera ya umoja wa Mashoga duniani...kiaina.

Ama kwa hakika njaa inaweza kukufanya ufanye mambo ya ajabu kabisa.
 
Back
Top Bottom