Chama cha Madaktari Tanzania (MAT): NHIF walikiuka makubaliano ya kamati ya kitita cha mafao cha mwaka 2023.

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT): NHIF walikiuka makubaliano ya kamati ya kitita cha mafao cha mwaka 2023.

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
MREJESHO WA KIKAO CHA DHARURA KATI YA NHIF NA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA- MAT
Utangulizi,
Tunapenda kuwafahamisha madaktari nchi nzima kuwa mnamo tarehe 10/07/2024 tulipokea barua ya mwaliko kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF yenye kumb.Na.EA35/269/01A/184,lengo kuu likiwa kufanya kikao cha pamoja ikiwa ni sehemu ya maelekezo ya uongozi wa Wizara ya afya kwa NHIF baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali zilizoonekana kufuatia maboresho yaliyofanywa katika kitita kipya cha mwaka 2023 yaliyoanza kutumika Julai mosi, 2024. Agenda kuu ya kikao hiki ilikuwa malipo ya ada ya usajili na ushauri wa Daktari (CONSULTATION FEE).

Ujumbe wa MAT uliongozwa na Dr. Deusdedit Ndilanha- Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT), akiambatana na Dr. Alex Elifuraha Msoka -Daktari bingwa wa upasuaji na mjumbe wa Baraza la Madaktari Tanzania (MAT), Dr. Onesmo Kisanga - Daktari mshauri wa magonjwa ya Figo na Rais-NESOT, Dr. Bita Muhanuzi Daktari bingwa wa magonjwa ya Dharura na muwakilishi-EMAT na Dr. Germana Vincent -Katibu TDA.

UFAFANUZI WA NHIF JUU YA AINA ZA MAHUDHURIO-CLINICAL VISITS

Kwa Mujibu wa taratibu za mfuko na aina ya mikataba ambayo mfuko umeingia na watoa huduma, kuna aina zifuatazo za mahudhurio (Visits: New visit, Refill visit, follow up visit, Normal visit,Emergency visit, Referral visit, Investigation visit, incomplete visit na other visits).

Mbali na mahudhurio mengine ambayo hayakuonekana na changamoto kubwa Chama kilifahamishwa kuwa kulikuwa na maboresho katika mahudhurio yafuatayo: New visit ambayo itakuwa ikilipwa asilimia mia moja (100% of consultation fee), Follow up visit ambayo italipwa asilimia hamsini (50% of consultation fee) na Refill visits- haitalipwa (0% consultation fee).

HOJA NA MSIMAMO KUTOKA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA (MAT)

1. Chama kiliueleza uongozi wa NHIF kuwa hakitambui refill visit kwani kwenye kamusi na taaluma ya udaktari haipo. Kuhusu follow up visits, ni sawa na mahudhurio ya kawaida (Normal visit) hivyo basi inastahili kulipwa yote kwa asilima mia kwani wanufaika wanapitia hatua zote za kimatibabu.

Sambamba na hili, MAT imeshauri ada ya kumuona Daktari ilipwe kulingana na kada ya Daktari aliyemuona, Hivyo tumeuomba uongozi wa NHIF ufanye marejeo ya mikataba walioingia na watoa huduma na kuboresha kipengele hicho. AIDHA tumesisitiza kuwa ada ya kumwona daktari ni heshima ambayo Daktari anapewa na jamii na haithaminishwi na kiasi kinachotolewa na mfuko hivyo tunaomba iheshimiwe.

2. Chama kimependekeza kwa NHIF wafanye mafunzo ya kuwajengea uwezo zaidi wawakilishi wa NHIF (Desk officers) kwenye vituo vya kutolea huduma ili kuongeza ufanisi, heshima na staha ya namna ya kuhakiki wanufaika wa mfuko pindi wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za matibabu, sambamba na hilo maamuzi ya mgonjwa aonwe na Daktari wa kada gani yaachwe ndani ya mamlaka ya mgonjwa mwenyewe (Patient autonomy) au Daktari na sio kama ilivyo sasa ambapo Desk officers wa NHIIF hutoa token ambazo huamua aina ya hudhurio na daktari wa kumuona.

Tumesisitiza kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na hawa maofisa kwenye hivi vituo, mfuko uhakikishe wanafanya majukumu ya uhakiki wa wanunufaika tu na sio majukumu ya Daktari kwa minajili ya kulinda faragha ya wanufaika (CONFIDENTIALITY).

3. Kuna idadi kubwa ya wagonjwa ambao changamoto zao zinawalazimu kupata huduma za
kibingwa/bingwa bobezi kila mara wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma (clinics). Chama kinaona ni muhimu waonwe na madaktari bingwa husika ili kuwa na mwendelezo wa matibabu na kupata uimara wa afya zao.

Mathalani wagonjwa wa renal transplant,liver transplant, Valve replacement na wengine wenye mfanano kama huu, hawa lazima waonwe na madaktari bingwa wa eneo husika bila kujali amekuja kama mgonjwa wa follow up ama hudhurio la kawaida.

4. Mapendekezo ya mabadiliko ya ada ya kumuopna Daktari yatasababisha wataalam wengi kuacha kutibu na wengine wameshaacha, vituo vingi hasa vya binafsi kushindwa kujiendesha na hivyo kuongeza changamoto zaidi ya ukosefu wa watoa huduma za afya ambao kimsingi hawatoshi.

5. Chama kimeomba uongozi wa NHIF kusimamia viwango vya ada pendekezwa na maboresho mengine kama tulivyokubaliana kwenye kamati ya kitita cha mafao cha mwaka 2023, kufanya mabadiliko yeyote ni kukiuka makubaliano ambayo yalichukua muda mrefu kufikiwa na kuafikiwa na makundi yote ya wadau kwenye sekta ya afya.

6. Chama cha madaktari Tanzania tunawaomba wakurugenzi taasisi za afya na wakuu wa hospitali kwa kushirikiana na NHIF wawe na utaratibu wa kutoa ufafanuzi wa kimkataba hasa vipengele vyenye ukakasi na vinavyogusa taaluma na wanataaluma ili kuwapa uelewa wa Pamoja kwa manufaa ya sekta nzima ya afya.

UONGOZI WA NHIF ULIPOKEA MAONI NA MAPENDEKEZO YETU KWA AJILI
YA KUWASILISHA KWENYE MAMLAKA ZA MAAMUZI KWA MABORESHO.


HITIMISHO
1. Chama kinaona kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu umuhimu wa kuwa na mfumo wa ugharamiaji huduma za afya ambao ni endelevu (sustainable health financing system) ili kuwepo na mawanda mapana zaidi ya namna ya kutoa huduma yenye masharti shirikishi.

2. NHIF ni bima yetu watanzania na Madaktari ni wadau muhimu sana, hivyo Madaktari wanaombwa kuzifuatilia taarifa zake kwa kina, tuilewe NHIF kwa undani na kwa wenye maoni au mapendekezo yenye lengo la kuiboresha wanaweza kuwasilisha maoni hayo kwenye vyama vyao vya kitaaluma (specialized associations) au moja kwa moja MAT na yatafikishwa NHIF.​

Tunawatakia kazi njema.
IMENDALIWA NA MAT MAKAO MAKUU

Goal "Promote and safeguard professionalism and medical practice in order to enhance a healthy Tanzanian society".​

20240715_162027.jpg


20240715_162031.jpg
 
Back
Top Bottom