Chama cha Mapinduzi kimekumbatia umimi kimeacha Demokrasia

Chama cha Mapinduzi kimekumbatia umimi kimeacha Demokrasia

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Mchakato wa kupata wagombea ndani ya Chama cha Mapinduzi umekuwa wa hovyo kuliko ubaya wa chama chenyewe.

Uwezi kuwa na chama Cha siasa kinachoendeshwa kwa hisia za kikundi cha watu, chama cha siasa kinaendeshwa kwa sheria, kanuni, na taratibu

Leo hii hofu ya chama kukimbiwa na wagombea na kwenda upinzani kumekifanya chama kushindwa kutoa majina ya wagombea kwa wakati.

Kuogopa watu kukihama chama wagombea wanatishwa na kutakiwa kukubaliana na mtazamo wa Mwenyekiti huku ukiaminishwa kwamba zipo kazi nyingi serikalini utapangiwa hivyo uwe mvumilivu.

Vigezo vya kuwapitisha wagombea havipo wazi, Kama Mwenyekiti alipatikana hadharani, kama wajumbe walipiga kura adharani nani anasema ana nguvu kuliko wajumbe na hiyo nguvu anaitoa wapi?

Leo hii wagombea udiwani wanapigwa ngumu ukiuliza kwanini, utagundua hawakubaliki.

Lakini pia huu mfumo umewasaidia watoto wa watu flani flani kuelekezwa kuchukua fomu na kwamba watapita tu.

Wapo watu wanapitia njia hii kuwapa wapenzi wao ujira, wapo watu wanakwenda na kisasi kupendekeza flan akatwe, wapo watu wanatoa ahadi kwa viongozi za kuwapa fedha au hata Mali lakini wapite au wapendwa wao wapite.

Mfumo unaondoa watu kujiamini na kuwafanya kuwaona watu wote wanaofanya kazi makao makuu ya chama Kama miungu watu.

Hakuna anayehoji, hakuna anayempinga Mwenyekiti wala hakuna chombo kinachomgusa mla rushwa ambaye yupo ndani ya ccm

Haya yanayofanywa na viongozi wakijiaminisha kwamba wanadola na wanatumia dola kutawala yanakiondoa chama mikononi mwa wanachama na kukipeleka mikononi mwa viongozi.

Najiuliza Kama uteuzi unafanywa kwa haki, kwanini hakuna mgombea aliyepita kwenye kura za maoni kati ya waliounga mkono juhudi? Kutokupita kwao si ishara kwa Mwenyekiti kwamba watu mliowapokea hatukubalini na dhulumu iliyotumika?

CCM INAKUFA, INAONDOKA KWENYE MIKONO YA WANANCHI, INASAMBARATIKA KWA SABABU YA KUVAA KOTI LA DOLA. DOLA SIKU ZOTE NI DHULUMA NA DHULUMA SIKU ZOTE UGEUKA UHASI
 
Toka Mzee magufuli amepewa uongozi ccm imebadilika kutoka kuwa Chama cha siasa kuwa Chama dola,hakuna tena mstari wa kuvitenganisha. Hii inasababisha chama kiendeshwe kama serikali ambapo wanachama wa kawaida wanapoteza sauti na kuishia kuwa na vinyongo.
 
Inabidi wajitathmini baada ya uchaguzi manun’guniko ni mengi sana na process yenyewe ya kukatana aipo wazi ni vigumu sana hilo zoezi kuitwa fair.

Huku kwingine unajiuliza captain Komba kawakosea nini asikiki kabisa na kawaachia nyimbo nzuri za campaign.

Hapohapo kuna waziri Mpina kipindi cha kufanya ziara za ‘charm offensive’ kama waziri mkuu anavyojaribu kuwakufurahisha wafanya biashara. Yeye Mpina yupo kwenye ziara ya kuudhi wapiga kura. Kuna mambo mengine wanasiasa wanasubiri uchaguzi upite kwanza.

Tatizo la Tanzania kuna asilimia ndogo sana ya wanasiasa katika watu wanaofanya siasa.
 
Kama mtu anadiriki kusema kupitishwa kuwa mgombea wa ccm inategemea siku hiyo kaamkaje hapo kutakuwa na demokrasia kweli
 
Mbona CHADEMA chako 'Kimekumbatia' sana pia Ukilimanjaro, Uarusha, Usingida na Utanga kidogo lakini huwasemi na huwashangai? Acha Unafiki!
 
CCM inaondolewa kutoka mikononi mwa mafisadi kurudishwa kwa wananchi wenye chama chao. Kelele kama hizi hatuwezi acha kuzisikia.
 
Toka Mzee magufuli amepewa uongozi ccm imebadilika kutoka kuwa Chama cha siasa kuwa Chama dola,hakuna tena mstari wa kuvitenganisha. Hii inasababisha chama kiendeshwe kama serikali ambapo wanachama wa kawaida wanapoteza sauti na kuishia kuwa na vinyongo.
Sikupingi mkuu
 
Back
Top Bottom