SI KWELI PreGE2025 Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya chaandika barua kukemea ukiukwaji wa Kanuni na Maadili ya Uongozi ndani ya chama

SI KWELI PreGE2025 Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya chaandika barua kukemea ukiukwaji wa Kanuni na Maadili ya Uongozi ndani ya chama

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
CCMMBEYA26JUL2025.jpg
 
Tunachokijua
Madai
Inadaiwa kuwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya kimewasilisha kwa masikitiko makubwa, malalamiko na tuhuma nzito dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama, Ndugu Dr. Emmanuel John Nchimbi, kwa vitendo vinavyokinzana moja kwa moja na misingi, taratibu, na kanuni za uongozi ndani ya CCM.

Barua hiyo inadai, kwa sasa, Ndugu Nchimbi anashikilia nafasi mbili kwa wakati mmoja:
1. Katibu Mkuu wa CCM - nafasi ya kiutendaji na kiutawala ndani ya chama

2. Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM

Hii ni hali ya mgongano wa wazi wa maslahi (conflict of interest) na inakiuka misingi ya uadilifu wa kiuongozi ndani ya chama chetu.

Pili, tuhuma za msingi zinazoibuliwa na wanachama na viongozi dhidi yake ikiwa ni pamoja na:

1. Kutumia ofisi ya Katibu Mkuu kuingilia mchakato wa uchaguzi wa ndani, kwa kutoa maelekezo kwa Kamati za Siasa za Wilaya na Mikoa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Mbeya, kuleta majina ya wagombea wanaomuunga mkono kisiasa na kimaslahi binafsi.

2. Kuweka shinikizo kwa viongozi wa Wilaya na Mikoa, kuhakikisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali yanapangwa kwa misingi ya kumuimarisha yeye binafsi kama mgombea mwenza, badala ya kuzingatia sifa, uwezo na ridhaa ya wanachama.

3. Kuasi mamlaka ya Mwenyekiti wa Chama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia kivuli cha nafasi ya Katibu Mkuu ili kuendesha ajenda zisizokubaliana na mwelekeo wa chama.

Kwa mujibu wa Barua hiyo, aliyeiandika na kusaini ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Dkt. Stephen Mwakajumilo.


Je, ni upi uhalisia wa barua hiyo?

Katika kutafuta uhalisia, ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa barua hiyo si ya kweli ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijatolewa na Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya.

Hata hivyo Barua hiyo haijasainiwa na Mwenyekiti wa sasa wa Chama hicho Patrick Mwalunenge bali Dkt. Stephen Mwakajumilo ambaye kwa sasa si Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya.

Aidha, akizungumza na JamiiCheck, Dkt. Mwakajumilo amesema "Siijui barua hiyo ndio kwanza nasikia kwako. Siogopi kutoa maoni, CCM tuna nafasi nyingi vikiwemo vikao, lakini siyo kutoa maoni mitandaoni."

​
Back
Top Bottom