McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Chama cha National League for Democracy (NLD) kitaanza kikao cha siku mbili cha Kamati Kuu kesho Jumatano, Julai 1, 2026 jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kinajiri wakati hali ya kisiasa nchini ipo katika mjadala mpana wa zuio la mikutano ya hadhara lililotangazwa wiki iliyopita, hatua iliyotajwa na Serikali kuwa ni tahadhari ya kiusalama nchini.
Soma Pia: Chama cha NLD chaionya CHADEMA, Chamshauri Msajili wa vyama kutosita kuchukua hatua ikibidi akifunge au kipigwe faini
Katika taarifa yake, Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma wa chama hicho, Pogora Ibrahim leo Jumanne, Juni 30, 2026 amesema kikao hicho kitahusisha wajumbe wa kamati kuu pamoja na viongozi wengine wa chama.
Katika taarifa hiyo, Pogora amesema kikao hicho kitajadili tathmini ya hali ya chama baada ya uchaguzi, hali ya kisiasa nchini, ujenzi na uimarishaji wa chama pamoja na mafunzo kwa viongozi.
Source: Mwananchi