PreGE2025 Chama cha siasa cha Wakulima (AAFP) chamteua rasmi kada wake, Kunje Ngombale-Mwiru kuwa mgombea wa urais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Chama cha siasa cha Wakulima (AAFP) leo kimemteua rasmi kada wake, Kunje Ngombale-Mwiru kuwa mgombea wa urais atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Hata hivyo, chama hicho kimeshindwa kumpata mgombea urais upande wa Zanzibar baada ya aliyekuwa anawania nafasi hiyo, Said Soud kupigiwa kura nyingi za hapana.

Hivyo, uongozi utalazimika kuitisha mkutano mkuu maalumu utakaoketi kumchagua na kumpitisha mgombea mwingine atakayepeperusha bendera ya chama hicho upande wa Zanzibar.

Katika uchaguzi huo uliogubikwa na vimbwanga vya aina yake, Kinje alichaguliwa baada ya kupata kura70 kati ya 97 zilizopigwa huku washindani wake wawili ambao ni Kilasa Mohamed, akiambulia kura sita na Fatuma Geheka kura sita pia na tano zikiharibika.

Katika mkutano mkuu huo maalumu, uliokuwa unaangaliwa kwa karibu na Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza, kada Kinje ataambatana na mgombea mwenza wake aliyepitishwa na mkutano huo, Chuma Mohamed.
image_2025-04-30_100933674.png
 
View attachment 3320317
Aanze sasa kujiandaa kuapishwa
 
Ndio maana jina Rais halina heshima siku hizi. Inabidi liongezewe vikorombwezo kama Dokta.

Nakumbuka zamani ilitosha tu kusema, NDUGU RAIS, NDUGU WANANCHI.

Baadae ikaja, MHESHIMIWA RAIS, NDUGU WANANCHI

Kisha tena MHESHIMIWA RAIS DOKTA/PROFESSOR, NDUGU WANANCHI

Sijajua hapo ni jina la rais kukosa heshima, au ni nini....
 
Samahani kwa anefahamu hawa wajomba ruzuku yao inakuwa ni bei gani?😂😂
 
Mgombea Urais kupitia Chama cha Allience For Africa Farmers Party(AAFP) , Kunje Ngombale Mwiru amewashukuru wanachama na wajumbe wa chama hicho kwa kumchagua kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu huku akitaka amani itawale.

Shukrani hizo amezitoa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mbali na kuwashukuru wajumbe na wanachama ameishukuru pia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kusimamia zoezi la kupitisha mgombea katika mkutano mkuu maalum wa chama hicho uliofanyika April 29, 2025 Temeke Jijini Dar es Salaam.

FB_IMG_17463802227582756.jpg
 
View attachment 3324692
Nchi inataniwa sana hii,eti mgombea urais?
 
Chama cha siasa cha Wakulima (AAFP) leo kimemteua rasmi kada wake, Kunje Ngombale-Mwiru kuwa mgombea wa urais atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Hata hivyo, chama hicho kimeshindwa kumpata mgombea urais upande wa Zanzibar baada ya aliyekuwa anawania nafasi hiyo, Said Soud kupigiwa kura nyingi za hapana.

Hivyo, uongozi utalazimika kuitisha mkutano mkuu maalumu utakaoketi kumchagua na kumpitisha mgombea mwingine atakayepeperusha bendera ya chama hicho upande wa Zanzibar.

Katika uchaguzi huo uliogubikwa na vimbwanga vya aina yake, Kinje alichaguliwa baada ya kupata kura70 kati ya 97 zilizopigwa huku washindani wake wawili ambao ni Kilasa Mohamed, akiambulia kura sita na Fatuma Geheka kura sita pia na tano zikiharibika.

Katika mkutano mkuu huo maalumu, uliokuwa unaangaliwa kwa karibu na Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza, kada Kinje ataambatana na mgombea mwenza wake aliyepitishwa na mkutano huo, Chuma Mohamed.
View attachment 3320317
Yaani huyu ndio unamwambia sasa mzee kunje ushindi ni wako..
Anaweza lia nakusema mimi nilikuwa natania tu .
 
Jamaa anapita mulemule kwenye nyayo za Mwiru
Yaani majina yote kaamua kuchagua kunje akaribie na ukoo wa ngombale…
 
Back
Top Bottom