Chama cha waamuzi wa England chakili kufanya kosa kuruhusu goli la Erling Haaland

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Chama cha Waamuzi cha England kimekiri kufanya kosa katika kuruhusu goli la ushindi la Manchester City dhidi ya Manchester United, ambapo Man City ilishinda 1-0 katika uwanja wa Old Trafford.

Katika taarifa iliyotolewa masaa machache baada ya ushindi huo wa Man City ilifichua kuwa imewasiliana na Man Utd na kukiri kuwepo kwa "kosa la kimaamuzi" na kwamba mwamuzi wa akiba wa video (VAR) "alipaswa kupendekeza mapitio ya tukio uwanjani" kuhusiana na goli hilo la ushindi la Erling Haaland.

Goli la mshambuliaji huyo mwanzoni lilikataliwa uwanjani kwa kuwa alionekena kuzidi (offside) kabla ya VAR kubadilisha uamuzi huo.

Maafisa wa VAR waliona kuwa Haaland hakuwa offside kutokana na nafasi ya beki wa Man Utd, Patrick Dorgu.

Hata hivyo, mchezaji wa Man City, Enzo Fernandez, alikuwa katika nafasi ya offside wakati akijaribu kuucheza mpira kabla haujamfikia Haaland.

Licha ya kutouguza mpira, msogeo wa Fernandez ulionekana kuathiri ulinzi wa mchezaji wa Man Utd, Lisandro Martinez, kabla ya Haaland kufunga mpira huo akiwa katika nguzo ya nyuma, jambo ambalo kwa mujibu wa sheria za mchezo lilipaswa kufanya goli hilo liendelee kukataliwa.

Msemaji wa chama hicho alisema: "Kufuatia tukio la dakika ya 60 katika mchezo wa Ligi Kuu Siku ya Jumapili kati ya Manchester United na Manchester City uliopigwa Old Trafford, tunaweza kutoa ufafanuzi kuhusu goli lililoruhusiwa la Erling Haaland, kuwa kulikua na dosari ya kimaamuzi."
1789369680592.png
 
View attachment 3670199
Nakumbuka Man U aliwahi pewa penati na VAR baada ya mechi kuisha.
 
Ingekuwa ni Bongo wangesema GSM anaua ligi yetu.
 
Back
Top Bottom