A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mtumishi katika halmashauri ya Kibondo.
Khero yangu kubwa ni Makato yanayokatwa na Chama cha wafanyakazi TALGWU, ambayo kwa kila mwezi ninakatwa 17,660/=
Ila ni miaka zaidi ya 2 imepita bila kusomewa Mapato na Matumizi katika Chama, je! Ukaguzi wa ndani na nje ya Halmashauri wanalitambua hili?
Na kama linafahamika kwanini hatupewi maelezo juu ya matumizi ya pesa tunazokatwa hata kupitia magroup au Notice Board?
Tunapoteza Iman na viongozi kwa sababu, hatujui makato yanagawanyika vipi na yanatumika vipi.
Na inapofika siku ya wafanyakazi naletewa T-shirt, kofia na Kalenda. Je! Katika 211,920/= kwa mwaka ndio tudanganywe hivyo?
Wakati naripoti nilipewa form tu kwamba jaza. Sikupewa hata chaguo la kujiunga Chama ninachokitaka kama ilivyo haki ya mtumishi wa umma.
Na pale unapoomba kutoka Chama kimoja kwenda kingine unazungushwa tu hupewi jibu la maana, zaidi ya kuambiwa "vyama vyote vinafanana tulia"
Ushauri wangu:
kama mtumishi ana haki ya kuchagua Chama cha wafanyakazi anachokitaka, basi nipewe muda na uhuru Na haki ya kuchagua na sio unaripoti tu kazini Na form unapewa bila hata kupewa maelekezo ya nini Na kwanini unajaza form hiyo.