Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT)-Kipo?

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488
Kuna nyuzi na mabandiko kadhaa ya masuala ya ufugaji hapa Jukwaani.

Na kwa wingi wa maelezo ya wafugaji hapa jukwaani na kwenye mitandao mingine nauona umuhimu wa kuwa na Chama cha wafugaji nchini ili wasemewe mahitaji Yao na mapendekezo Yao hasa katika kuimarisha umoja na Amani baina Yao na wakulima na raia wengine.

Kama Chama Hiki kipo basi tunaomba tupate ufafanuzi wanajishugulisha na nini katika kutimiza matakwa ya kuendeleza ufugaji Bora na wenye faida kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla.

Kama Chama hakipo basi kianzishwe ili kutimiza lengo lililoelezwa hapo juu.

Natanguliza Shukrani kwa yeyote atakayetoa ufafanuzi.

Karibu.
 
Mkuu unazungumzia chama cha wafuga nini? Majini, ndevu au mifugo?
 
Sidhani kama kuna Chama cha wafugaji ambacho ni general,lakini Kwa chama kimoja kimoja cha wafugaji mifugo vipo,mfano chama cha wafugaji nguruwe na chama cha wafugaji mbuzi kibiashara.
Asante sana, Mkuu. Naweza kupata anwani kamili ya vyama hivi kama vimesajiliwa rasmi na Mamlaka za serikali. Pia na uongozi wa vyama hivyo, bila kusahau katiba ya vyama hivyo?
 
Hiki chama husikika wakati wa uchaguzi tu kwani wanachama wake ni wakijani.
 
Asante sana, Mkuu. Naweza kupata anwani kamili ya vyama hivi kama vimesajiliwa rasmi na Mamlaka za serikali. Pia na uongozi wa vyama hivyo, bila kusahau katiba ya vyama hivyo?
Kama hicho chama cha wafugaji nguruwe ni kimesajiliwa rasmi na kinaitwa(TAPIFA)na wamejitoa kutoka kwenye chama cha wafugaji Tanzania (ccwt) baada ya kuona ccwt ipo lakini kama ipo jina tu,Yani Bado inafanya kazi Kwa kusuasua na kushindwa kuwafikia wafugaji wengi yani vilevile kama ilivyokuwa Kwa taasisi nyingine za mifugo kama Tvla,Taliri,Lita,bodi ya nyama,bodi ya maziwa
 
Asante sana kwa ufafanuzi, Mkuu. Taarifa yako hii ni muhimu Sana.
 
Chama kipo sema kama alivyoelezea Toofast hakisikiki sana. Nadhani watakuwa na uchaguzi wa viongozi CCWT ngazi ya Taifa mwezi huu au ujao mwanzoni. Kwa hali niionayo sasa kinakuja kwa kasi sana baada ya kujua kuna walioasi na kuanzisha hicho cha nguruwe. Kipo vizuri kwa sasa kwa sababu ngazi hizo za juu kina wanazuoni wengi sana
 
Uchaguzi itakuwa mwezi huu classmate zangu wa Olevel walipiga chini kuendelea na shule wakaingia ufugaji na Kilimo na wamepata vyeo ngazi ya wilaya Mhasibu na Katibu wa chama wilaya wanakula posho za chama tu.
 
Nadhani watakuwa na uchaguzi wa viongozi CCWT ngazi ya Taifa mwezi huu au ujao mwanzoni.
Asante sana, Mkuu kwa taarifa hii. Nimechakurachakura taarifa mtaa wa wa mitandaoni, nimepata taarifa kuwa Leo unafanyika uchaguzi wa Kanda ya Mashariki wa Chama Hiki, na kesho unafanyika uchaguzi wa Taifa wa Chama.

Ngoja niendelee kufuatilia.
 
Nahitajia kuanzisha chama cha polygamist,kama kipo pia naombenj utaratibu wa kujiunga.
 
Nahitajia kuanzisha chama cha polygamist,kama kipo pia naombenj utaratibu wa kujiunga.
Ni wazo lako umelitoa. Hivyo, nashauri nalo ulifungulie uzi mpya ili wazo lako hilo lionekane kwa urahisi na upate maoni mengi ya kukusaidia kulitekeleza wazo lako. Kwenye uzi huu hutapata maoni kwa urahisi. Huu ni ushauri wangu.
===
Tukirudi kwenye mada iliyopo mezani. Tupe habari yoyote inayohusu Chama Hiki cha wafugaji ambacho umedhitishiwa kipo na kwa mwezi huu kinaendesha uchaguzi.
 
DODOMA: TUME ya Uchaguzi ya Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) imewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya Taifa ndani ya chama hicho kufanya kampeni zenye staha ambazo hazitaleta vurugu wala kuwagawa wafugaji nchini

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Chama hicho, Charles Malangwa wakati akitoa taarifa Kuhusu mwenendo wa uchukuaji fomu na urejeshaji kuelekea uchaguzi wa Aprili 8, Mwaka huu.

“Huko wanakojinadi ni vyema wakazingatia maadili ya chama chetu, watengeneze kampeni za kistaarabu, wajenge wanachama wetu kwa sababu watakapoendesha kampeni zenye mwelekeo mbaya watawagawa wanachama hawa mwisho wanakuja kuwaongoza haohao” Charles Malangwa

Mlezi wa chama hicho, Joseph Makongoro ametoa nasaha kwa wagombea na na viongozi wa Tume ya uchaguzi kuhakikisha wanaendesha uchaguzi wa huru na haki bila kuvunja katiba ya Chama Hicho

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania CCWT, Mrida Mshota, ambaye ni miongoni mwa wagombea na nafasi hiyo ameeleza baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja tangu ashike kijiti cha uongozi

“Wafugaji wapatao 8413 wameanza kupatiwa mikopo kutoka kwenye mabenki mbalimbali na kutuwezesha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuuza mazao yatokanayo na mifugo nje ya Nchi yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 50, kwa mana hiyo kazi iliyofanyika ni kubwa” alisema Mrida Mshota.

Chama cha wafugaji Tanzania kinatarajia kufanya Uchaguzi mkuu Aprili 8, Mwaka huu Jijini Dodoma

 
Wafugaji waliojitoa ni wengi tu ,Tena wengi ni wale wenye vision kubwa na pesa ,na wameamua kuanzisha vyama vingine au association nyingine za ufugaji mfano kuna hawa wanaitwa Tanzania goat farmers association(TAGOFA) wameanzisha hii association baada ya kuona hawapati msaada wowote kutoka CCWT kama vile msaada wa mbegu bora,halafu kama ilivo ada ,Ujinga wa nchi yetu unajulikana kwamba Kuna watu wanakaa sehemu fulani Kwa ajili ya upigaji tu na si Kwa ajili ya masilahi ya nchi,ndo maana si ajabu kukuta hicho chama kimejaa madaktari ,maprofesa maybe kutoka sua ambao walitakiwa wawe na mchango mkubwa katika kusukuma gurudumu la ufugaji wenye tija lakini mwisho wa siku hamna chochote siasa tu ,kama taasisi nyingine za mifugo kama tvla,taliri,Lita,sua,etc jinsi zilivyojaa siasa.

Yote Kwa yote kichocheo kingine Cha kufanya haya mabaya kuwepo kwenye sekta ya mifugo ni kwamba sheria bado haifanyi kazi inavotakiwa kwenye nchi yetu hususani kwenye swala la matibabu,uzalishaji,ustawi wa mifugo(animal treatment,production and welfare) na vile vile hakuna mgawanyo wa majukumu yaani (specialization of labours) mfano kama Kwa Tanzania veterinary laboratory agency(TVLA) na Tanzania livestock research institute(TALIRI)wamejazana madaktari ,wakati kiuhalisia wapo vijana walio wazuri kimaarifa(knowledgeable and competent) wa faini ya Veterinary Laboratory technology ambapo kiuhalisia ndo sehemu Yao ya kufanyia kazi lakini mwisho wa siku wanapigwa vita Kwa sababu ukicheki hata Baraza la veterianri la Tanzania ,limeshikiliwa na hao hao madaktari Kwa sababu wanajua Kuna ulaji ,Kwa hiyo wameweka ulaji mbele kuliko maslahi ya nchi ,ndo maana hata kulikuwa na hati hati ya kuifuta kozi ya maabara ya mifugo(Veterinary Laboratory technology) kutokana na kuona kwamba kama haina tija kwenye upande wa ajira na vilevile haijulikani sana Kwa watu ,Kwa sababu aliyekuwa anafundisha wataalamu wa maabara ni Livestock training agency(Lita) na sehemu Yao ya kufanyia kazi ni hapo Tvla na taliri
 
Kwa maelezo haya ni kweli Chama kina changamoto. Nimejaribu kufuatilia habari za Chama Hiki cha CCWT nikuwa kimeboresha katiba hivi karibuni; bahati mbaya sijaipata hiyo katiba.

Nikiipata hiyo iliyoboreshwa nitaangalia kama maboresho yaliyofanywa kwenye katiba kama yamejikita kutatua changamoto ulizozieleza.

Mkuu Asante sana.
 
Kwa maelezo haya ni kweli Chama kina changamoto. Nimejaribu kufuatilia habari za Chama Hiki cha CCWT nikuwa kimeboresha katiba hivi karibuni; bahati mbaya sijaipata hiyo katiba.
Nikiipata hiyo iliyoboreshwa nitaangalia kama maboresho yaliyofanywa kwenye katiba kama yamejikita kutatua changamoto ulizozieleza.

Mkuu Asante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…