Ni wazo zuri utakutana na wafugaji wa kuku wa kienyeji tulioanza na kuku wawili leo nina zaidi ya mia moja........kuna uzi humu wa ufugaji kuku uliyeanza ufugaji utafute utapata uzoefu mkubwa........wewe ulieanza na kuku hamsini pambana na hao kuku kwa kuzingatia chanjo ili wakuwe maana ni kazi kubwa kwa mtu anayeanza kuanza na vifaranga .....
ni wazo zuri ila kuna mtu kaanzisha na ametualika tujiunge umoja wa wafugaji wa kuku wote kwa ujumla. Mnaonaje tukiingia humo?
Asante kwa ushauri vp upo dsm naomba uniuzie japo kuku5 majike wa size ya kati kama inawezekana mkuu
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Jamani nikaribisheni kwenye mabanda yenu nije nipate japo elimu kidogo nitashukuru,jana nilikua Morogoro maeneo fulani nikakuta watu wanafuga kuku wa asili sana nimependa tatizo hawataki kuuza ni PM kama upo tayari kunisaidia
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Karibu Morogoro ......swala la kuuza kuku wakubwa huwa ni nadra sana
Ndugu wana Jf amani iwe nanyi.kwa mda mrefu nimesoma maandiko kadha wa kadha juu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji humu Jf na nimehamasika.kwa kuanzia na kwa mazingira niliyopo nimeanza na kuku 50 wa kienyeji . wiki ijayo nitaongeza kuku 100 .sasa baada ya kusoma post tofauti tofauti juu ya mbinu anuai ningependa kushauri tuanzisheni chama cha wafugaji kuku wa kienyeji.hii itakuwa na faida zifuatazo kwa uchache ;(1) kubadilishana uzoefu na mbinu za ufugaji bora (2) kujenga mtandao wa masoko.karibuni kwa mjadala tuboreshe wazo hili.