KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Chama cha waganga wa tiba asilia Mkoa wa Simiyu, Machi 12, 2023 kimefanya Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wake, ambao watakiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano.
Hata hivyo baada ya uchaguzi huo, swali kwa watu wengi limekuja Je? Chama hicho kimegeuka kuwa cha kisiasa?
Tunajua kazi ya tiba asilia ni kazi ya kitaalaamu zaidi lakini kwa Mkoa wa Simiyu yawezekana chama hiki kimegeuzwa kuwa cha kisiasa na kutoka katika utalaamu wake.
Hoja hii inatokana na viongozi waliochaguliwa, kuwa na vina saba na chama cha kisiasa lakini siyo vina saba tu, ni viongozi ndani ya chama kimoja kikubwa hapa nchini cha kisiasa.
Mwenyekiti wa chama hicho cha watalaamu hao wa tiba asilia aliyechaguliwa ni Mayunga Kidoyai.
Mayunga huyu ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mbali na kuwa kada Mayunga ni Katibu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCMM) katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.
Licha ya kuwa mtendaji aliyeajiriwa kwenye Chama hicho, Mayunga ni mkazi wa Simiyu.
Mbali na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho cha tiba asilia aliyechaguliwa naye ni kada mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi na ni kiongozi wa kisiasa kupitia CCM.
Makamu Mwenyekiti anaitwa Gambanga’di Kaliba, huyu ni Diwani (CCM) wa Kata ya Mwhanuzi iliyoko Wilayani MeatuMkoani Simiyu.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe kwenye mkutano huo, ni viongozi pia wa CCM, mmoja wapo wa viongozi hao ni Katibu wa uhenezi CCM Wilaya ya Itilima Magombe, huyu ni mjumbe kwenye chama hicho.