Chama Cha walimu Tanzania (CWT) VS Chama Cha kutetea haki za walimu Tanzania (CHAKUHAWATA)

Chama Cha walimu Tanzania (CWT) VS Chama Cha kutetea haki za walimu Tanzania (CHAKUHAWATA)

Usipojiunga what’s next?
Usipojiunga kwa hiyari basi utaungwa kwa lazima, na kama ni mwalimu basi automatically CWT.

Kujiunga vyama vya wafanyakazi ni kwa mujibu wa sheria.
 
Hao jamaa kwa kitendo cha kugomea nafasi waliopewa na mh Rais kwenda kumsaidia kutekeleza ilani ni tatizo kubwa sana.
Na chakushangaza maafisa utumishi katika Halmashauri mbalimbali nchini wanawaunga mkono hao majamaa kwa kuisapoti CWT.
Wanaikandamiza CHAKUHAWATA ambayo kimsingi ipo kumsaidia mtumishi kwa ada nafuu za uanachama.
CHAKUHAWATA mwalimu mwanachama huchangia kiasi cha shilingi 5000 kwa mwezi pasi kujali kiwango cha mshahara wake.
CWT mwanachama huchangia kiasi cha shilingi 8000 hadi zaidi ya shilingi 40000 kulingana na kiwango cha mshahara kitu ambacho ni mzigo mkubwa kwa mtumishi.
Ukizingatia kuwa kanuni za ajira na mahusiano kazini zinampa uhuru mwajiriwa kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi lakini kwa walimu imekuwa tofauti.
Kujiunga na CWT imekuwa lazima ukishaajiriwa tu wanakuunga.
Sasa kuna ulazima gani kulazimisha uanachama kwa chama ambacho kinampinga mh Rais kwa kukataa hata teuzi zake jambo ambalo ni dharau kubwa wameonyesha waziwazi viongozi hawa wa CWT kwa kiongozi wa nchi.
Tunawaatarifu maafisa utumishi wapeni uhuru wao wafanyakazi wa kujiunga na chama cha wafanyakazi wanachokitaka wao.
Ahsante.
 
Back
Top Bottom