Chama cha Walimu Zanzibar: Tuna uhaba wa Walimu wa Sayansi, wanaohitimu wanakwenda wapi?

Chama cha Walimu Zanzibar: Tuna uhaba wa Walimu wa Sayansi, wanaohitimu wanakwenda wapi?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Chama cha Walimu Zanzibar kimehoji Wanafunzi wanaohitimu na kufaulu masomo ya Sanyansi katika Skuli za Unguja na Pemba wako wapi baada ya kumaliza kusoma kwani bado kuna changamoto ya uhaba wa Walimu katika masomo hayo.

Hoja hiyo imeulizwa mbele ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika mkutano wa tisa wa Chama cha Walimu Zanzibar katika Ukumbi wa Taasisi ya Utalii Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja, jana Agosti 13, 2025.

Rais wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU), Mwl Seif Mohammed Seif amesema katika Shule za Secondari kumekuwa na Walimu wanaosomesha kidato cha 4 na huyohuyo anasomesha kidato cha sita jambo linalowafanya Walimu kufanya kazi zaidi ya uwezo alionao.

Aidha Seif Amesema hii inatokana na masilahi ya walimu kutorizisha na kuwafanya wanafunzi kutovutiwa na kada hiyo.
 
Back
Top Bottom