Chama cha Wamiliki wa Malori chapinga Kamata Kamata ya Malori, Watishia Kuendelea kupaki Malori

Chama cha Wamiliki wa Malori chapinga Kamata Kamata ya Malori, Watishia Kuendelea kupaki Malori

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
21 August 2026

DEREVA ALIA NA SERIKALI|| AWAPA MBINU MANISPAA MNAKOSEA, AOMBA TANZANIA IFUATE MBINU ZA NCHI YA ZAMBIA KUPATA UTATUZI ENDELEVU


View: https://m.youtube.com/watch?v=pLViMXXsr3Y

Dereva wa malori yanayovuka mipaka aelezea jinsi nchi Zambia walivyojipanga vizuri kwa kuwa na sehemu kibao za layover / sehemu za malori kupaki kando ya njia kuu / highway kwa ajili ya madereva kupumzika na pia kuyafanyia ukaguzi malori yao wanapokuwa ktk safari ndefu.

Kwa mtindo huo nchini Zambia foleni ya magari kupaki kando mabarabarani au katika service road hakuna na pia wanakuwa na usalama wa mizigo yao.


TOKA MAKTABA :
30 Julai 2026


FOLENI IKIZIDI WATU WATA LIKIMBIA JIJI LA DAR ES SALAAM " RC ALBERT CHALAMILA"

View: https://m.youtube.com/watch?v=5yE2j1858wA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameagiza kuanza kwa operesheni maalum ya kufungua maegesho (lorry reserves) yote ya malori kuanzia wiki ijayo ili kupunguza msongamano na kuboresha huduma katika Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza Julai 29, 2026 wakati wa ukaguzi wa mizani ya Malawi Cargo bandarini, RC Albert Chalamila amesema malori yote yanapaswa kuegeshwa kwenye maeneo rasmi na Serikali itaweka utaratibu wa muda wa kuingia na kutoka ili kuongeza ufanisi wa usafirishaji.

Pia amesisitiza matumizi ya teknolojia ya kisasa ikiwemo mizani ya kielektroniki na mifumo ya kamera, akieleza kuwa viongozi wa mkoa wanapaswa kutatua changamoto za wananchi badala ya kusubiri kila jambo liamuliwe na Serikali Kuu.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elius Lukumay amesema wanapinga kamata kamata ya malori inayoendelea, na kwamba wako tayari kupaki malori kama hali hiyo itaendelea.

Soma Pia: ~

View attachment 3652824

18 August 2026

FULL INTERVIEW / MAHOJIANO KAMILI

TATOA Yalalamika Tamko la Kukamatwa kwa Malori


View: https://m.youtube.com/watch?v=uOBulXyDwKQ
Tanzania Truck Owners Association (TATOA) imeeleza masikitiko yake kuhusu tamko la kukamatwa kwa malori yanayoegeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Press Conference ya dharura iliyofanyika leo katika ofisi za TATOA zilizopo JM Mall, Mwenyekiti wa TATOA ameeleza umuhimu wa ushirikiano uliopo kati ya TATOA na wadau mbalimbali katika kutafuta suluhisho la changamoto ya msongamano wa malori jijini Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom