Boveta
JF-Expert Member
- Jul 23, 2019
- 3,174
- 3,804
Chama Cha Wananchi CUF jana kupitia Baraza Kuu la Uongozi lilimchagua Bi. Husna Abdallah kuwa katibu mkuu wa chama hicho.
Hivyo katika medani za siasa hapa Tanzania, Bibi Husna anakuwa ndio Mwanamama wa Kwanza kushika nafasi hiyo lakini pia hii inaonyesha jinsi Chama Cha Wananchi (CUF) kilivyo na uwazi inapotokea mwanachama mwenye sifa anapotaka kugombea nafasi yoyote.
Aidha Bi. Husna alishinda kwa kura 19 wakati mpinzani wake ndugu Ali Abarani alipata kura 11.
Chama cha Wananchi (CUF) kimedhamiria kufanya mambo makubwa katika Uchaguzi ujao wa Uraisi, Wabunge na Madiwani October Mwaka huu.