Fursa ya kupata Katiba mpya mliharibu ninyi wanasiasa baada ya kususia ushiriki kwa sababu za kibinafsi ambazo wananchi hawakuwatuma seuze kongamano hilo ambalo bila shaka ni kichaka cha kujifariji.
Tume huru ni ipi? kama tume itaundwa na wajumbe toka vyama washirika wa siasa vilivyosajiliwa hiyo sio tume huru tena ila ni kutengeneza kikundi cha mabishano kwa kuzingatia ushabiki wa itikadi. Kama tume itaundwa kutokana na watu wenye taaluma kwa kuomba nafasi za kazi basi tutegemee mamluki wengi kuingizwa humo ili malengo ya upande wenye nia OVU ufanikishe zoezi hilo.
Duniani kote hakuna tume huru zote ziko compromised ila ulimbukeni wa baadhi ya wanasiasa wanadhani ndio itakuwa nafuu kwao kukwea ngazi kufika juu ya kilinge.