Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) kimewataka wananchi kuwa makini na watu wanaotoa huduma za kisheria bila ya kuwa mawakili(maarufu kama vishoka) ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Malipo ya Pamoja na Mapambano Dhidi ya Vishoka (anti vishoka) Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Sweetbert Nkuba amesema wananchi wasishawishike na bei ndogo wanazopewa na watu hao
Akibainisha athari zitokanazo na vishoka Wakili Nkuba amesema ni pamoja na kuchafuka kwa taswira ya sheria kwani wananchi wanakosa imani kwa kwa taaluma hiyo kutokana na uzoefu mbaya wanaopata wa kutapeliwa.
Athari zingine aliazoainisha Nkuba ni pamoja na kudumazwa kipato na hali ya maisha ya mawakili halali, kukwamisha maendeleo ya taifa,kufifisha nidhamu ya kitaaluma.
Ametoa wito kwa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Msajili wa Hati ni kuhakikisha ukaguzi wa risiti za EFD zinazoambatana na mikataba kuhakikisha zina shabihiana na bei halisi zilizopo kwenye mikataba
Kuanzia leo Juni 18, 2025 TLS imezindua kampeni ya kupambana na vishoka hao huku wakishirikiana na jeshi la polisi na taasisi zingine za kisheria kudhibiti watu hao