Chama cha Wanasheria (TLS) mngependekeza aina ya uvaaji (dress code) katika mikutano yenu

Chama cha Wanasheria (TLS) mngependekeza aina ya uvaaji (dress code) katika mikutano yenu

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
282
Reaction score
561
Nimeangalia mkutano uliyojumuisha uchaguzi wa raisi wa chama cha wanasheria kwenye vyombo mbali mbali vya habari.

Tukio hili kubwa la kitaifa lilifanyika Arusha kwenye jumba kuu la mkutano al maarufu kama AICC ni ukumbi wa mkutano ambao hufanyika mikutano mikubwa ikizingatiwa Arusha ni Makao Mkuu ya jumuia ya Afrika mashariki, nimesikitika kuona hawa ndugu zetu “wasomi” wakiingia mkutanoni na kila aina ya vazi wengine wamediriki kuvaa na makofia kama wanamuziki binafsi nikiwa mtaalamu wa Masuala fulani nasema hiyo siyo sawa.

Wanasheria hujitapa kwamba tendo ambalo halijaainishwa kwenye kanuni na adhabu siyo kosa lakini kitendo cha kuingia AICC na jinzi mlegezo na kapelo kama wahuni hii halipendezi, kwenye ulinzi tunasema “where there is a crowd of people with common interest there must be uniformity to reduce anonymity “ naomba kuwasilisha.
 
3502E280-6A9A-446D-BA14-2ABAE66215C6.jpeg
 
Back
Top Bottom