Chama kikiwafukuza Wabunge Viti Maalum CHADEMA itakuwaje?

Chama kikiwafukuza Wabunge Viti Maalum CHADEMA itakuwaje?

DUMPER

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2017
Posts
568
Reaction score
945
Badala ya kulalamika na kutukana na vilevile waandishi wetu kuogopa na kukaa chini sisi...Tumefanya utafiti mdogo kwanini ghafla Bunge na mfumo mzima wa uongozi wa serkali ya Tanzania ghafla wanawahitaji hao wabunge wa CHADEMA.

MASHARTI YA PESA TOKA NJE (DONORS)
Kama mnaelewa bunge letu hakuna pesa la kuliendesha na ndo maana kuna wabunge tumesikia wamelalamika hawajapewa pesa za magari. Kwahiyo Bunge linahitaji pesa toka nje na wameandika maombi kwa donors wao wakubwa na wameletewa mashariti madogo ili hiyo pesa ipatikane.

Diversity and Inclusion in Tanzania Parliament
Pamoja na demokrasia mbovu iliyozaa hilo bunge,Donors wamesema wanaweza kutoa hizo pesa kama tu shariti la bunge kuwa diversity and inclusivity (sijapata maneno mazuri kwa Kiswahili).Bunge diversity and inclusivity kwa mujibu wa donors ni Bunge lenye;

1.Wabunge toka vyama mbalimbali vya kisiasa

2.Wabunge wanawake toka vyama mbalimbali vya kisiasa au makundi ya kijamii.

Bunge la Tanzania linatakiwa kukizi 4 protected characteristics kati ya 9 za kawaida ambazo ni 1.Age 2 gender 3.sex orientation na 4 disability

JOB NDUGAI
Huyu anaelewa kinachoendelea na anautaalam mzuri wa mabunge ya madola na Zaidi zaidi anazihitaji hizo pesa kwa nguvu zote ili kuendesha bunge na anawahitaji kwa nguvu zote wale wanamama wa chadema ili kutiki box zote za mashariti ya pesa,sasa ni rafiki mzuri sana wa Halima Mdee.

HALIMA MDEE
Huyu ni muhimu sana kwa Ndugai na mfumo mzima kwasababu yeye anaweza kutiki box zote hapo juu.
 
Dona kantri kuhangaikia tilioni mbili? Mpaka wamejidhalilisha kweli? Dunia nzima imeshajua wameghushi pmaka watoa hell wamejua , Kati ya heshima na msaada tutasimamia heshima? In Kabudi's voice, kiko wapi hata wiki hazijaisha wanakimbizana na tilioni mbili za LAAC na PAC conditions to get loans.
 
...
HALIMA MDEE:

Huyu ni muhimu sana kwa Ndugai na mfumo mzima kwasababu yeye anaweza kutiki box zote hapo juu.
Halima Mdee anaweza ku-tick box zote hapo juu! Age; Gender; Sex Orientation; Disability? Fafanua.
 
Habari wanajamvi.

CDM kupitia KM wao wanasema hawakupeleka orodha ya majina ya Wabunge wa viti maalumu NEC. Tumeshuhudia Wabunge wateuliwa wa viti maalumu 19 wakiapishwa.

Tetesi ni kwamba Bunge linalazimisha uwepo wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ili wapate pesa kutoka kwa wahisani wetu Triliioni 2. Bila hizo pesa inasemekana Bunge litakuwa kapuku, Wabunge wataishi kama Walimu na huenda wakaibana serikali kisawasawa.

Sasa najaribu kujiuliza maswali ambayo nayaleta kwenu tujiulize kwa pamoja.

CDM wakiweka ngumu na kuwafukuza uanachama hao wateule 19 ambapo kisheria watakuwa wamepoteza uhalali wa kuwa Wabunge. Je, Bunge na serikali watafanya nini ili kunusulu hizo Trillions za pesa zisipoteee?

Wanaweza kufukuza Wabunge kadhaa wa CCM ili warudi kwenye uchaguzi na kuielekeza tume iwapitishe wapinzani kuwa Wabunge?

Je, huu uhusiano wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni na msaada wa hayo mapesa haukujadiliwa kabla ya uchaguzi? Walijisahau au walishindwa vipi hata kupitisha Wabunge kadhaa hata wa chama kingine tofauti na CDM ili wakaunde kambi rasmi ya upinzani. I think it was simple Technic kuliko sasa hivi tunapoonekana watu wasiostaarabika.
 
Wanawahitaji wanawake wa CDM kwasababu ni wanawake.
Nalog off!!
 
Mtu mmoja ambae ni head master wa chama ndio chanzo cha yote hayo. Lkn sasa ni nani wa kumfunga paka kengele? Kila mtu anaishia kuja huku JF kulalamika tu
 
... Halima Mdee anaweza ku-tick box zote hapo juu! Age; Gender; Sex Orientation; Disability? Fafanua.
Dude yeah Mlizie komrade ndugai......she is full " Diversity and inclusivity"
 
Wamelikoraga, wacha walinywe.

Na huu ujinga unaoendelea hauwezi kuwashawishi wahisani zaidi ya kuona haya ni maigizo na watayapuuza.

Mabavu bila akili ndio yamezaa yote haya.
Wamerikoroga, kwakua mke wako hajapata nafasi, angekuwemo mke wako ungekaaa kimyaaa. Acheniii unyanyasaji wa kijinsia.
 
Back
Top Bottom