Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA Watangaza Wiki ya Mashujaa wa Demokrasia Tanzania, Kilele Septemba 07

Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA Watangaza Wiki ya Mashujaa wa Demokrasia Tanzania, Kilele Septemba 07

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328
Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA Watangaza Wiki ya Mashujaa wa Demokrasia Tanzania, Kilele Septemba 07

Chama kikuu cha upinzani Tanzania, CHADEMA kupitia uongozi wake imetangaza Septemba 1 mpaka 7, kuwa wiki ya mashujaa wa kidemokrasia, ambapo kilele chake itakuwa ni Septemba 07, 2025.

Siku hiyo imetengwa ikiwa ni siku ambayo kiongozi wa chama hicho, Tundu Lissu, alinusurika kuuwawa baada ya kushambuliwa kwa risasi mnamo Septemba 07, 2017. Lakini pia ndiyo siku ambayo mwili wa mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA, Ali Kibao mwili wake ulipatikana baada ya kutekwa na watu wenye silaha mwaka 2024. Katika matukio yote mawili, polisi wameendelea kueleza kuwa wanachunguza.

Katika siku ya kwanza ya maadhimisho hayo, mwanasheria Tito Magoti ameongoza kampeni ya mtandaoni #IamTunduLissu, #MiminiTunduLissu, ambapo pamoja na mjadala uliofanyika mchana, watumiaji wa mitandao wameendelea kusambaza habari kuhusiana na Tundu Lissu, ambaye toka Aprili 10,2025, yupo rumande kwa kushitakiwa makosa ya uhaini.

CHADEMA watafanya Baraza la mtandaoni mnamo Septemba 02, 2025, ambapo mijadala mbalimbali itafanyika.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, mnamo Septemba 07, 2025, bendera za chama hicho zitapepea nusu mlingoti nchi nzima kuwakumbuka wanachama wao na wapigania demokrasia waliofungwa, kutekwa, kupotezwa na hata kuuwawa Tanzania. Shughuli hiyo itaenda sambamba na ibada, na mijadala ya kisiasa, na majadiliano nchi nzima.
 
Baada ya uhuru, hatukutarajia mambo ya aina hii? ila CCM ndio wametufukisha hapa.
 
Baada ya uhuru, hatukutarajia mambo ya aina hii? ila CCM ndio wametufukisha hapa.
Je maombi
Kulalamika mitandaoni
N.k

Unafikiri hizo njia zitaleta mabadiliko yoyote ?

Nadhani ni bora chadema watumie mbinu ya Super sub zaidi .

Yaani waautazame mchezo pasipo wao kucheza then wakiingia uwanjani wafanye kweli .

Ila hawatoweza kutegemea fair play kutoka kwa Ccm ambao na wao wanahitaji kitu kilekile wanachokihitaji Chadema.
 
Back
Top Bottom