Kiwalani finest
Senior Member
- Jul 6, 2024
- 116
- 85
Mheshimiwa Mchungaji,
Najaribu kufikiri tu mifumo yetu ya kiutawala.
Chama kinachoshinda ndicho huunda Serikali na kuisimamia.
Zamani hatukuwa na wasomi, kwa sasa wasomi wapo — tatizo ni kubebana katika kupeana position kunafanya wenye kustahili kuachwa na wasiostahili kupenya.
Tiba ya haya ni kuondoa uoga na kisha kupeana makavu bila chenga.
Mfano:
Nilitamani sana tuanzie kwenye chama, tukisikia mtu kakiuka mifumo, zinaitishwa katiba, kanuni, miongozo na taratibu — anasomewa, anachukuliwa hatua huku akiona ya kuwa haonewi.
Kisha tuje kwenye Serikali.
Vile tunavyoshangilia kibaka akifungwa kwa wizi wa kuku, vivyo hivyo kwa viongozi wenye makando kando nao wachukuliwe hatua.
Kisha kama kuna watumishi labda waliishia darasa la tatu halafu walidanganya wakapata vyeo — watolewe, watafutiwe kazi za ukuli bandalini kulingana na elimu zao, ili zile nyadhifa walizozikalia kwa janja janja na rushwa zipate watu sahihi.
Tukifanya hivi:
Ilani ya CCM:

- Kwanza, nchi itabarikiwa sana.
- Pili, tutakuwa tumeitendea haki Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
- Ibara 26(1)(2)
- Ibara 12(1)(2)
- Ibara 13(1)(4)(5)
- Ibara 09 (a, b, f, na h)
- Ibara 29(1)(2)
Ilani ya CCM:
- Ukurasa 01, Ibara 04
- Ukurasa 161–168
- Ukurasa 08, Ibara 10 na 11