Chama Kipya: New York Metropolitan Tanzanians Community

- Sasa mkuu naomba uwataje wenye harufu na ubalozi ili tujiajngalie kama ni kweli, ninakuruhusu uwataje hao unaodhani wana harufu ya ubalozi.

William.


Wakuu Malecela & FMEs,
Hivi mnafikiri kuna mTZ anayechukia tukipata chama cha kutujumuisha huku nyikani?

Kwanza ni kitu cha kushangaza sana na kusikitisha kuona kuwa waTZ wa jiji kama la NY na vitongoji vyake mpaka leo hii hawana jumuiya yao licha ya wingi wao katika hayo maeneo.

Lakini inaelekea tatizo sio waTZ bali ni baadhi tu ya watu wanaotaka kuanzisha vyama kwa maslahi yao binafsi halafu inaelekea hawambiliki.

Mkuu Malecela, wewe mwenyewe ambaye mke wako ndio mtumishi wa muda mrefu kuliko wote hapo ubalozini NY, sijui unategemea tukueleweje unapokuja na tangazo kuwa eti;
  1. Mmeshapewa rukhsa na Balozi kuanzisha chama na chama kimeshaandikishwa na wewe ambaye ni mtegemezi wa ubalozi ni mmoja wa viongozi.
  2. Katiba na Website ya chama tayari viko mbioni sijui nani anayevigharimia wakati wanachama hawajakutana?
  3. Hukutueleza ni jinsi gani mlivyokutana mkaamua kuanzisha chama kwa ajili ya waTZ wote bila kuwashirikisha hao wanaotakiwa kukimiliki chama.
  4. Hukutufahamisha kuwa ni nani na vipi mliteuliwa kuwa viongozi, wasifu wenu ni upi n.k, hata kama nyie ni viongozi wa muda (interim). Hapa mnaonekana kujiona kama vile mko above all other TZs ambao mnategemea kufuata mnachowaeleza tu. This is a typical behavior of waungwana serikalini, something that we are all very much familiar with.
Watanzania tunataka kujumuika kwani tunaelewa jumuiya itatusaidia sana kwenye masuala mbalimbali ya kijamii na labda hata kuisaidia nchi. Lakini kama chama kitaanzishwa kwa mizengwe na mazingira ya kutatanisha, msije mkashangaa historia ikajirudia. WaTZ hatutaki kuwa ni rubber stamp ya maamuzi yenu nyie wa ubalozini/serikalini.
 
 
 
sometimes huwa napata tabu sana kuwaelewa watanzania.........
 
 





Malecela,
You completely missed my point. Read again my postings (one added above). There was nothing against you personaly untill when you and FMEs demanded that I put down some names of individuals with close relations with the embassy's staff.

Kwa wewe kujuana na akina JK na kuwa na spouse ubalozini, sidhani kama ni kitu cha kushangaza hasa ukitilia maanani kuwa mwenzetu umebahatika kubeba jina bora la familia (Malecela). Hiki ni kitu ambacho hakuna anayeweza kukuondolea and you have all the right to be proud of and use it effectively.

Lakini unapokuja na kutueleza kuwa wewe ndio kiongozi mwanzilishi wa jumuiya tena kwa mazingira ya utata, nafikiri Mtanzania yeyote mwenye akili timamu na aliyeona jinsi mtandao wa JK ulivyojipanga TZ na abroad na kuiharibu nchi, lazima apandwe na jazba na munkari na kutaka kujua vipi kunani kwenye jumuiya ya NY?

Hakuna aliyesema kuwa chama kisiwe na mahusiano na ubalozi au na serikali ya TZ maana hili haliwezekani. Wala sidhani kama kuna aliyesema kuwa chama kiwe na nongwa na JK.

Bali, sidhani kama ni dhambi kujaribu kuondoa mapema miingiliano ya kimaslahi kwenye uongozi wa chama ili kuhakikisha kuwa chama kinawatumikia WaTZ na sio serikali/ubalozi.

Kwani kuna ubaya gani kwa watumishi wa ubalozini na familia zao wakawa wanachama wa kawaida tu na sio viongozi ili kuondoa uwezekano wa kuozesha masilahi ya chama na ya mwajiri wao?
 
 

- Again, ninaomba kusema kwamba katika hiki chama, hatutambui members kwa ubora au ubovu wa familia walizotoka, sijui kama New York tuna wananchi ambao wametoka familia bora na wengine wakatoka familia mbovu, I find this to be very insulting na ni simply lugha ya kibaguzi, unajua sasa ninaanza kuelewa ni kwa nini vyama vingine huko nyuma vimeshindwa kusimama, inaonekana kuna ka-element ka - ubaguzi ubaguzi hivi, huu nao Mkuu utanisamehe sana kwamba kama ule ushauri wako wa kwanza sitaufikisha kwenye chama kwa sababu una harufu ya kibaguzi, tofauti kabisa na msimamo wa hiki chama kipya, hatujali rangi, elimu, familia, jina wala kazi ya mwananchi wote wanaruhusiwa kushiriki maana ni Jumuiya yao.

Ahsante


William. (CO).
 
Lakini unapokuja na kutueleza kuwa wewe ndio kiongozi mwanzilishi wa jumuiya tena kwa mazingira ya utata,


- Mkuu hiki chama kimeanzishwa na wengine, yaani msingi wake uliwekwa na wengine ambao baadaye walinifahamisha kama na wewe ulivyofahamishwa, mimi kama members wengine wote niliitwa kwenye mkutano ambapo ulifanyika Harlem, siku ya Jumamosi wiki ya mwisho ya February last month, katika ule mkutano nikaombwa na wananchi waliohudhuria kushiriki katika uongozi wa muda wa hiki chama kwa hiyo again naomba uondokane na haya mawazo ambayo ni uzushi na hayawezi kutusaidia hiki chama kusonga mbele, unaonekana unazo potentials tena kubwa sana kukichangia hiki chama ushauri wa maaana kuliko huu uzushi uzushi na ubaguzi baguzi.

nafikiri Mtanzania yeyote mwenye akili timamu na aliyeona jinsi mtandao wa JK ulivyojipanga TZ na abroad na kuiharibu nchi, lazima apandwe na jazba na munkari na kutaka kujua vipi kunani kwenye jumuiya ya NY?

- M-Tanzania yoyote mwenye akili timamu anatakiwa kupandwaa na jazba na munkari, kusikia kwamba kuna chama cha wananchi kinaanzishwa lakini hakitaki members wenye ndugu serikalini, wala marafiki ambao ni viongozi wa taifa, na kwamba hakitaki members wanaotoka kwenye familia bora, ni lazima wawe wanatoka kwenye familia mbovu. Bado ninatatizwa sana na hizi kauli zako Mkuu. Hayo mengine ya mtandao sisi hiki chama hayatuhusu kabisaa naomba nikuachie mwenyewe.


- So far dhambi niliyoiona ni ushauri wa kibaguzi na name calling bila substance wala facts, hakuna maingiliano yoyote ya kimasilahi kati ya serikali na wananchi wake wanaoishi nje ya chi, infact ni mawazo finyu sana haya hata kuyasema in the public, licha ya kuyatoa kama ushauri wa kukiimarisha chama kipya cha wananchi walioko nje ya nchi, sijui wewe mkuu sisi wengine hatuna uadui na serikali yetu, wala wafnaya kazi wa serikali yetu, au hata ofisi zetu za ubalozi huku nje hatuna uadui nazo, ndio maana ninasema kwamba huu ushauri hatuutaki na wala hatutausikiliza kabisa, maana ni nothing but ubaguzi.

Kwani kuna ubaya gani kwa watumishi wa ubalozini na familia zao wakawa wanachama wa kawaida tu na sio viongozi ili kuondoa uwezekano wa kuozesha masilahi ya chama na ya mwajiri wao?
[/QUOTE]

- Mkuu umejitahidi sana kuonyesha kwamba ni dhambi kwa mwananchi kuwa mwanachama wa hiki chama huku akiwa mfanyakazi wa serikali au hata mwenye ndugu huko, lakini in the end ni nothing but ubaguzi tu, ambao hiki chama hakina nafasi nao kabisaa. Ninaomba nikuhakikishei kwamba katika huu ushauri wako hakuna hata moja tutakalolichukua, na ninakutakia siku njema sana mkuu.

Ahsante.


William. (CO).
 
Mkuu, nimekuwa nikisoma post zenu kwa umakini na kiundani, lakini bado sijona mambo yafuatayo:

The purposes of formation of the corporation and/or organization.

The lawful provisions, if any, for the conduct and regulation of the business/organization and affairs of the Corporation, for its voluntary dissolution, or for limiting, defining, or regulating the powers of the Corporation, or of its directors or members, or of any class of members.

Any powers limitation? Why? Is it possible for a person to be disqualified from holding any office by reason on any interest?

This corporation is formed under what section? Namaanisha is it a charitable, scientific, etc, what does the Articles of Organization says?

Who has power to amend the articles of organization? Is it by vote? Kwa pasenti ngapi? Memba wa aina gani wana haki ya ku-vote?

Je, kutakuwa na prescribed dues? If yes, how did you guys come to that number/amount? If, no, why?

What are the objectives of the corporation/organization?

Je, hii organization itakuwa na Executive Committee? Ya watu wangapi?

What will be the duties of the executive committee?

With what approval of the Council, the individual members may have to establish chapters for the furtherance of the objectives of the Society/Organization? Is there such a clause kwenye Article ya Org?

Tuanze na hayo mkuu William M. CO
 

- Mkuu wangu Max, heshima sana kwa huu ushauri wako mzito sana ni kwamba ninaomba muda kidogo nizipitie nukuu zote nilizonazo, kuna zenye majibu ya baadhi ya maswali yako na mengine najua for a fact kwamba hatuna ndio maana tumekuja hapa kujitambulisha na kuomba ushauri, ndio maana nilisema huko nyuma watu wenye experience za u-CEO kama wako, tunawahitaji sana katika hiki chama hasa katika kuweka msingi na muongozo wa hiki chama kipya, sasa tuongozane ndugu yangu Max.

Ahsante.


William.
 
I will try to speak with you, this week-end. Be blessed.
 

William,

Naona umeanza mbio za Obama kwa kuwa community organizer kwi kwi kwi kwiiii!!..... big up kwa sana!
 
Ninaomba nikuhakikishei kwamba katika huu ushauri wako hakuna hata moja tutakalolichukua......

Ahsante.

William. (CO).
Mkuu Malecela,
Nashukuru kwa majibu yako mazuri. Lakini naona hatutafika popote na hili maana hatujadili tena hoja bali sasa inaonekana kama na wewe binafsi umekuwa ni hoja.

Nia yangu ilikuwa kujadili conflicting interests kama watu wa ubalozini watakuwa ndio viongozi wa jumuiya ya WaTanzania, especialy when we take into consideration of our current nepotic and sycophantic political environment.

But because we seem not able to have a discussion, then may be we can just wish well our new association. I believe we can always come back to this topic in the future if I somewhat become prophetic. Chiao.
 

- Ilitakiwa kuwa discussion, lakini ukaigeuza kua a Jerry Springer's like act, lakini kama sasa umekubali kwamba ulikuwa nje ya mstari ninashkuru sana na soon nitaleta mengine zaidi ya kuhusu chama kipya, ahsante sana mkuu na it was nice having a debate with you na karibu sana ujiunge na chama na ikibidi ugombee uongozi wa kudumu itakapofika time.

Ahsante.


William. (CO)
 
Hili tangazo la William Malecela na reactions kutoka kwa wasomaji wake, vimenifanya nipeleleze kidogo ili kubaini kulikoni huko New York.

Nimebahatika kuchimba na kuyapata ya New York. Endapo ni ya uzushi tu, basi yatupilieni mbali. Lakini kama yana bifu yeyote kuhusu NY (na, pengine, kwenye jumuia nyingine za wa-Tanzania ughaibuni), inafaa sana kujizatiti katika kukabiliana na virusi vya mgawanyiko wa u-siasa, u-kabila na u-dini ili kuweza kujenga jumuia hizo kuwa chimbuko la utamaduni wa m-Tanzania, ughaibuni; kuliko kumeremeta ki-vyama vya siasa, kiu-kabila na/au ki-u-dini.

Enzi za Balozi wetu (wa Kudumu kwenye Umoja wa Mataifa) mmoja kulikuwepo na tetesi kuwa Mwalimu Nyerere alifikiria kuteua ma-Balozi waliokuwa wanachama tu wa CCM. Huo ulikuwa ni wakati wa ”Chama Kushika Hatamu” (Vanguard Party).

Walikuwepo wa-Tanzania waliokuwa wakifanya kazi kwenye Sekretariati ya Umoja wa Mataifa waliokuwa wanategemewa kwamba huenda Mwalimu Nyerere angewakumbuka na kuwazawadi na wadhifa wa kuwa ma-Balozi.

Baadhi ya wa-Tanzania hao walikuwa ni wazee: Dixon Nkembo na Asanterabi Nsilo Swai. Lakini wengine walikuwa bado vijana-jana: Remi Michael Tiruhungwa, Bernard E. Muganda, Leo Msuya, Joseph Kotta, C.S.M. Mselle, Ismat Steiner na Fortunatus Lwanyatika Masha. Kuna tetesi kuwa baadhi yao walitafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa ma-Balozi.

Hii haina maana kuwa kila mmoja wa hao wa-Tanzania alikuwa akiota kuwa Balozi siku moja; la hasha! Kwani wengine walikuwa wameishatengwa na TANU/CCM.

Waliofikiria kuwa huenda Mwalimu Nyerere angewakumbuka, walikimbia kimbia kuanzisha Tawi la CCM hapo New York kupitia Ofisi ya u-Balozi!

Na kweli Tawi hilo lilifunguliwa. Mwenyekiti wake alikuwa ni Mzee Dixon Nkembo. Mlezi wa tawi alikuwa ni Balozi. Lakini waliokuwa mbele kuanzisha Tawi hilo walisubiri bila Mwalimu Nyerere kuwakumbuka kuwa ma-Balozi. Njozi ya Tawi la CCM ikaishiwa mafuta; likafa!

Kundi lingine la wa-Tanzania wa NY lilikuwa ni la graduate wanafunzi wakisoma hapo New York University na Columbia University, ambao hawakupenda sana kuwa wanachama kwani walikuwa huko NY kwa muda tu. Uanachama wao ulibakia hapa hapa Tanzania.

Baadaye, likaja wimbi la “vijana”: Watoto wa ma-Balozi na watoto wa ”vigogo na wakubwa” kutoka Bongoland na kutua sehemu za Mt. Vernon. Wengine waliahama Tanzania kabisa na kumwacha baba yao huko Tanzania na kuanzisha nyumba yao mpya hapo Mt. Vernon – ingawa baba yao huwa anakuja kuwatembelea.

Watoto wa ma-Balozi (waliobaki huko Amerika wakati wazazi wanamaliza muda wao na kurudi nyumbani au wengine kubadili kazi na kujiunga na Sekretariati ya Umoja wa Mataifa) na wa ”vigogo na wakubwa” kutoka Bongoland walipenda kujumuka kwa kufanya parties zaidi kuliko kufikiria kuunda Umoja wa Jumuiya ya wa-Tanzania.

Kutokana na kundi hili kukutana kutana kwa ajili ya parties, walijitokeza vijana wengine wenye kutaka kuunda Umoja wa Jumuiya ya wa-Tanzania wa kudumu. Kwahiyo, kila mara walipokutana, suala la kutaka kuunda “Chama cha wa-Tanzania” huwa linaibuka na kutongoza akili zao.

Wa-Tanzania wengine huwa wanajiweka mbele mbele kutekeleza lengo hili la kuunda “Chama cha wa-Tanzania” kutokana na kuwa karibu karibu na Balozi, kupitia tabia ya ki-mtandao ya u-dini au u-kabila na/au vyote viwili.

Ya NY yanasisimua kweli! Balozi akiwa m-Islamu, wa-Islamu wengi wanajitokeza kutoka kila mahali NYC na vitongoji vyake. Hii ilikuwa wazi sana wakati wa enzi za ma-Balozi wa-Islamu. Kuna wakati mmoja nyumba ya Balozi ilikuwa kama Msikiti siku ya Ijumaa.

Wenye kujua hayo majambo wanaeleza kuwa kulikuwepo na wakati m-tanzania mmoja (nasikia kuwa sasa ni Alhaj) na kijana mwingine wa kutoka sehemu za Boston (nasikia ana cheo cha Maalim) walijifanya kama kiungo cha wa-Tanzania hapo NY, ikiwa ni pamoja na William Malecela kuwa, pia, mbele, kama “Community Organiser” wa wa-Tanzania.

Habari hizo zinaelezea kuwa huyo wa Boston bado anavinjari vinjari NY kwa sababu ma-Balozi wawili waliofuatana wanatoka sehemu za kwao. Sijui kama NY ikipata Balozi mpya asiyetoka sehemu za kwao, huyo Boston ataendelea kufunga safari za kila mara kwenda NY!

Lakini ya NY yana harufu mbaya ya ubaguzi baguzi. Balozi akiwa m-Kristu, hivyo hivyo tena. Kuna Balozi m-Kristo mmoja, ambaye alipata kusoma huko huko New York aliunda mtandao wake na ma-rafiki walioselea na kuishi NY miaka mingi.

Wakati wa enzi za Balozi niliyemtaja paragrafu ya tatu mtandao wake ulivuka mipaka hadi Uingereza, ambako kulikuwa na kundi kubwa la wa-Arabu waliokimbia Zanzibar.

Kuna habari za kuaminika zenye kueleza kuwa baadhi ya wa-Arabu hao wa Uingereza walikuwa wakitumia Ofisi ya u-Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa katika kupata pasi mpya au kubadilisha zile zilizoishia muda wake. Badala ya kutumia Ofisi ya u-balozi wetu mjini London, walipendelea kupeleka pasi zao mjini New York!

Zaidi, kuna pia habari kuwa kulikuwa na binti wa ki-Sukuma aliyepata mchumba mzungu, m-Diplomasia wa Australia. Binti huyo alikuwa akiishi kwa muda nyumbani kwa m-Pemba wa kutokea sehemu za Mwanza, rafiki wa Balozi huyo hapo Kurasini karibu na Bendera Tatu. Mchumba wake huyo alikuwa ahamishiwe huko Papua New Guinea. Huyo binti alitafuta pasi ya Tanzania bila kufanikiwa. Lakini alifanikiwa kupata pasi kutoka kwa Balozi huyo huyo iliyoandikwa huko New York!

Balozi huyo alipalilia sana mahali pa uzawa, ikiwa ni pamoja na kupendelea wa-Arabu wa Tanzania waliokimbilia huko Ulaya. Kwani kuna ukweli kuwa hao wa-Arabu wengine walikuwa hawabadilishi pasi zao huko waliko. Pasi zao zilikuwa zililetwa New York na kubadilishwa ikiwa ni pamoja na mpya kutolewa!

Wengi sana walimpenda Balozi huyo. Na wakati wa hafla walijazana hapo nyumbani 30 Overhill Road, MT. Vernon, NY 10552. Mtindo huo wa kuwaalika wa-Tanzania hapo nyumbani aliuendeleza Balozi m-Kristo, niliyemtaja hapo awali.

Kuna habari za kusisimua kwamba wakati wa enzi za balozi huyo wa-tanzania walicheza dansi hapo nyumbani wakikanyaga hayo mazulia na kukalia hivyo viti mpaka vikachoka. Washiriki wengine walipata breakfast hapo kuliko pengine kuendesha magari yao kurudi majumbani kwao na huku wamelewa chakari! That was a good idea!

Halafu alikuja Balozi m-Islamu mwingine. Hakuna aliyekanyaga hapo nyumbani. Balozi huyo alifuatiwa na ma-Balozi wengine wawili waliokuwa wa-Kristo, ambao walifungua mlango wa nyumba hiyo nyumba tena kwa wa-Tanzania, kupitia kwa vijana wao kujumuka na vijana wenzao kwa parties kwenye basement yake tu. Na wakati mwingine kukita hema hapo kwenye uwanja wa nyumba hiyo ya Balozi.

Sasa Melecela amejibatiza jina la Community Organiser ili kujionyesha kwa Balozi kuwa yeye (William) ni kiungo muhimu cha wa-Tanzania wa NY and its environs! Kuna sababu yake. Kuna sababu yake.

Kwa muda mrefu, hakuna hata m-Tanzania ambaye aliwahi kupewa kazi kama local employee, isipokuwa wafuatao:

Kuna kisa cha mama mmoja aliyekuwa Sekeretari wa Balozi kuenguliwa na
nafasi yake kuchukuliwa na mama m-Jamaika aliyehamishwa kutoka Ofisi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamaika Norman Manley na kuletwa hapo New York.

Hata hivyo, inashangaa kwa nini u-Balozi hautaki kumwajiri Sekeretari m-Tanzania (mzalendo) kwenye nafasi nyeti ya Sekeretari wa Balozi.

Wa-Tanzania wengine wa kundi la local employee ni mke wa Afisa wa u-balozi wa zamani ambaye sasa ameajiriwa na Sekretariati ya UN) na Khamis Sued (Khamis Kageshaki), ambaye kaka yake Sued alikuwa ni Afisa wa u-Balozi hapo New York na hapo baadaye Balozi.

Mwisho, ni mke wa William Malecela. kulingana na mtririko wa habari nilizopata, inaonekana, pengine, William anapalilia unga wake anaposema kuwa umoja-tegemewa wa wa-Tanzania Metropolitan NY umepata blessings za Balozi!

Hayo ya William Malecela ya kujiweka mbelembele (CO - Community Organizer) na msemaji wa wa-Tanzania) kupitia Ofisi ya u-Balozi wa Tanzania kwenye UM (Umoja wa Mataifa), sio mapya. Ana sababu ya kupalilia unga wa kazi kwa mke wake.

Na kama Balozi akitaka kuwaalika wa-Tanzania atatumia ma-Afisa wake, sio William Malecela.

Kwa nini William Malecela anawafanyia ma-Afisa wau-Balozi wajibu wao? Soma tangazo lifuatalo:

“Tangazo: Bash la Balozi NYC Haya Tukutane Wakuu! W. J. Malecela 11th August 2009, 03:10 AM: Wakulu wote JF, na wananchi wenzangu wote mnaoishi US na hata nje, na hasa New York City na vitongoji vyake...”

Ninaomba kuwekwa sawa, endapo habari hii niliyopata si ya kweli!
 

- Mkuu naomba utafute tangazo la majuzi la msiba wa Balozi Mwakawago, Professor aliyelitangaza amesema ni kwa niaba ya ubalozi NY kwa hiyo again ninasikitika sana kwamba badala ya nyinyi watu kama wewe muandishi mkubwa sana wa vitabu duniani kutusaidia ushauri wa kukisimamisha chama hiki cha wananchi, leo unajijngiza kwenye majungu na uzushi ambao hata kichwa hauna, hivi Tanzania tumelogwa na nani? Hivi wakati ninawasaidia vijana wasio na pa kulala mbona sikuwahi kusikia haya ya kujipendekeza?

- Jamani muwaonee huruma wananchi wenzenu ambao walijitokeza Harlem na kuanzisha rasmi hiki chama, mimi nitaendelea na juhudi zangu za kukitangaza hiki chama pamoja na haya majungu na uzushi maana tumeyazoea, ila inasikitisha yanaporushwa na wasomi, hapo ndio inatia kinyaa sana.

- Again mkuu hakuna ukweli wa haya maneno ila ni uzushi na uongo wa mchana, Mungu atujalie chama kitaendeelea Mwenyekiti wa muda anarudi jumatatu na akifika tu ataenda DC kutafuta baraka za Balozi na wazee wengine kule.

Ahsante Sana.


William. (Community Organizer)
 
Ninaomba kuwekwa sawa, endapo habari hii niliyopata si ya kweli!

- Mkuu nimejaribu sana kukusaidia ukweli maana uliyopewa yote ni uongo wa mchana na ni majungu, ninashukuru sana kwamba uliweka hili chana hapa kwamba huna uhakika na unachosema. Kwani wale wafanyajkazi wengien pale ubalozini wanapaliliwa na nani kuendeleza kazi zao?

- Sihitaji kufanya anything kupalilia kazi ya mke wangu ambayo amekua akiifanya toka akiwa Belgium, sasa alipokuwa huko alipaliliwa na nani? Mkuu achana na majungu haya yanaturudisha nyuma wa-Tanzania

Ahsante
.

William. (Community Organizer)
 
Date: Thu, 25 Feb 2010 16:48:02 -0500








- Mkuu Esteemed ninaamini utapitia matangazo yote hapo juu na kujionea mwenye uzushi uliouleta kwamba ni nothing but majumgu na uzushi na ndio unatukwamisha wa-Tanzania kila siku hatuwezi kusonga mbele majungu, majungu, chuki, wivu, fitina fitina maendeleo hakuna!

Respect.

FMEs!

 
hivi W Malecela na FMES sauti ya umeme wana uhusiano gani?
huu mjadala na ule mjadala wa baba mtu na Sofia Simba naona kama wana fanana.

Anyway hawa ndio waliotufikisha hapa tulipo, ni bora kuwapuuuza, hawana cha uzalendo wala nini. wanachumia matumbo yao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…