Observation yako ipo sahihi kabisa kiongozi. Performance ya msimu uliopita kwenye CCL iliwadanganya sana kuanzia viongozi, wachezaji, benchi la ufundi na hata mashabiki wa Simba ambao waliamini historia ndio itaamua mechi. Inawezekana Simba ingepangiwa na timu yenye jina kubwa Afrika na ikaingia kama underdogs wangeweza kufanya vizuri zaidi ya hivi kutokana na walivojijenga ki saikolojia
Kwenye usajili ndio walinishangaza sana maana wakarudia makosa yaleyale ya miaka yote ya kusajili kishabiki na kishamba bila kuzingatia mahitaji ya kiufundi ya timu. Bado tuna safari ndefu sana kwenye maendeleo ya vilabu vyetu maana resources nyingi zinatumika lakini bila weledi ni kuzipoteza fursa na rasilimali
Najaribu kufuatilia takwimu za simba za usajili kwa misimu mitatu mfululizo zinatisha sana.
2016-2017 walitumia approximately 500m
Wakawasajili.
Shiza kichuya
Mzamiru Yassin
Methid wanjali
Murshid Juuko
Lodit Mavugo
Vicent Angban
Bessala Bokungu
Na muivori coast mmoja aliishia kuwafunga mbao tu.
Baadae wakamuongeza
Danny Aggyei
James kotei.
2017-2018 walitumia approximately 1billioni
Kwa kuwasajili.
1Emanuel Okwi
2 Haruna Niyonzima
3 Shomari Kapombe
4 Ally shomari
5 Erasto Nyoni
6 John Bocco
7Aishi Manula
8 Yussuf Mlipili
9. Said Mohammed Nduda.
10 Asante Kwasi
11 Nicolas gyan
Msimu wa 2018-2019
Walitumia approximately 1.3b kwa kuwanunua
1 paschal Wawa
2 Rashid Mohammed
3 Marcel Kaheza
4 Adam Salamba
5 Meddie Kagere
6 Deogratius Dida
7 Zana Coulibally
8 Hassan Dilunga
9 Claotus Chama
2019-2020 wametulia approximately 1b +
Kwa usajili wa hawa.
1 Francis kahata
2 Deo kanda
3 Tairone Dasilva
4 Henrique wilker
5 Gerson Fraga
6 Eldin Shiboub
7 Ibrahim Ajib
8 Gadiel Michael
9 Beno kakolanya
10 Miraj Adam
11 Kennedy Wilson
12 Haruna Shamte
Kikosi hiki walichosajili msimu huu ukiondoa Miraji Adam wachezaji wengine waliobaki almost miaka yao ni 30 years kila mmoja haya ni matumizi mabaya ya akili na pesa.
Ukiangalia misimu yote hii mitatu simba wamefanya usajili wa wachezaji 10+ kila msimu bila mwendelezo wa kuboreka kwa kikosi hii maana yake simba wanasajili kwa mahitaji ya muda mfupi.
Uongozi wa simba usichokijua ni kwamba kikosi kilichofanya vizuri msimu uliopita kilikuwa pamoja kwa miaka miwili nyuma lakini msimu huu walifanya usajili wa kukusanya bila kuzingatia malengo ya muda mrefu ya timu.
Next season more than half ya squad ya simba watakuwa above 30
1 Nyoni
2 wawa
3 Bocco
4 deo Kanda
5,Chama
6 Shiboub
7 tairone Dasilva
8 wilker
9 Kagere
10 Kapombe
11 Shamte
12 Bocco
Hii maana yake tutegemee kuflop kwa viwango vyao tena je simba imejiandaa kufanya usajili wa billion + tena msimu ujao ?