Wydad imeshuka kiwango, hasa baada ya kuondokewa na wachezaji wake muhimu wa msimu uliopita. Simba wangeweza kufika nusu final kwa kupitia Wydad msimu huu kama sio ujinga wa bench la ufundi, uongozi wa Simba, Chama na Ally Salim.
Wydad waliokolewa na golikipa wao kudaka mikwaju 2 iliyopigwa vizuri na kapo Kapombe na Chama kitu ambacho Ally Salim hakuweza kukifanya kutokana na uchanga wake golini.
Uongozi wa Simba na bench la ufundi kuacha kumtumia Beno Kakolanya kwasababu za kijinga, kipuuzi, kibwege, unsporting na kichawi kukaa langoni kudaka penati na kumuamini kijana kinda kulisababisha Simba kuingia hasara kubwa sana ya kutolewa mashindanoni na timu dhaifu ya Wydad, Ningekuwa mimi ni mo ningemsaka aliyesema Beno kipa namba 2 asikae golini kwenye mashindano haya makubwa baada ya Manula kuumia.
Chama na Kapombe hawakuwa makini na kazi Yao pia ingawa penati huwa hazina mwenyewe lakini "why us" every day tutolewe robo final?
Bench la ufundi lilipaswa kumwingiza Beno kudaka japo penati TU badala ya mtoto Ally ambae aliteseka sana kujirusha chini kwa namna ileile kwa penalti zote.
Swali ni je, Simba itakuwa na ubavu wa kumzuia Inonga abaki Simba? Inonga pekee ndiye aliyepunguza idadi ya magoli siku Ile.