Chama ni chetu, serikali ni yetu, bunge letu, na spika ni wetu

Chama ni chetu, serikali ni yetu, bunge letu, na spika ni wetu

Bigirita

Platinum Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
16,039
Reaction score
7,465
Makamba kasema hiviiii!

CHAMA NI CHETU, SERIKALI NI YETU, BUNGE LETU, NA SPIKA NI WETU.

Bandugu, huyu mzee ana-akili timamu?
 
Makamba kasema hiviiii!

CHAMA NI CHETU, SERIKALI NI YETU, BUNGE LETU, NA SPIKA NI WETU.

Bandugu, huyu mzee ana-akili timamu?

Mkuu, Mh. Makamba kasema kipi cha ajabu hapo kuhusiana na hali ya kisiasa Tanzania mpaka unaulizia utimamu wa akili yake?!
 
kauli imetoka kibabe hio naona sema siwezi kushangaa manake siwezi kushangaa kauli hio kutoka kwa makamba manake jamaa liropokaji hovyo hovyo tu .
 
Chama ni chao, na serikali ni yao, lakini bunge si lao. Na spika si wao. Makamba hajui maana ya demokrasia na usimamiaji wake. Amezoea ubabe ubabe tu. Ndo mananga waliopo CCM hawa.
 
The problem is that God gave men a brain and a penis, and only enough blood to run one at a time.

Hii nayo imekaaje?
 
Anajaribu kujustify kile walichokifanya Dodoma na hata watu wakipiga kelele wao bado wameshika dola na hamuwezi kuwafanya lolote.
 
Makamba kasema hiviiii!

CHAMA NI CHETU, SERIKALI NI YETU, BUNGE LETU, NA SPIKA NI WETU.

Bandugu, huyu mzee ana-akili timamu?

Hajakosea kabisa hapo. Sisi waTZ wa kawaida hatuna chetu hapo kila kitu ni chao. Kama tunadhani bado tuna chetu nadhani sisi ndo itabidi tujiulize kama tuna akili timamu. Kila kitu kipo wazi kabisa.
 
vyote vya kwao lakini nchi ni yetu. jamani tuikomboe nchi yetu mwakani 2010 chonde chonde, tuwaache wabaki na vyao.
 
CHAMA NI CHETU, SERIKALI NI YETU, BUNGE LETU, NA SPIKA NI WETU.
Ukisikia mawazo ya Kidikteta ndio haya!... Inasikitisha sana kuona upeo mdogo wa viongozi wetu ktk maswala nyeti kama haya..
 
Spika ni mwanachama wa ccm ambacho ndicho kimeshika dola ama serikali kwa maana hiyo sehemu pekee ya kudhibiti nidhamu ya wanachama ni ni kwenye chama kwenyewe.

Kama mtu anataka Hasizibitiwe awe mgombea binafsi
 
Ukisikia mawazo ya Kidikteta ndio haya!... Inasikitisha sana kuona upeo mdogo wa viongozi wetu ktk maswala nyeti kama haya..

Mimi napenda sana viongozi wa juu CCM wanapolewa madaraka na kutoa maneno kama haya. Hapa wananchi wanakuwa na ufahamu kabisa kuwa wakiendelea kichagua CCM na kuwapa wabunge wengi ni hasara kwa Taifa. Uamuzi ni wao, wasije sema hawakusikia.
 
vyote vya kwao lakini nchi ni yetu. jamani tuikomboe nchi yetu mwakani 2010 chonde chonde, tuwaache wabaki na vyao.

tehetehe

wewe ni mwananchi? au mwenyenchi?

angalia usijekuwa unaota ndoto mchana
 
Spika ni mwanachama wa ccm ambacho ndicho kimeshika dola ama serikali kwa maana hiyo sehemu pekee ya kudhibiti nidhamu ya wanachama ni ni kwenye chama kwenyewe.

Kama mtu anataka Hasizibitiwe awe mgombea binafsi

Nidhamu ya mwanachama au spika? kama wanataka kudhibiti weanachama wao wanapotekeleza majukumu kwa mujibu wa katiba ya nchi, basi huo na ndio ni mwanzo wa mwisho wa udikteta.

Lakini sishangai, wanachofanya ni sawa na kukimbiza mwizi ukiwa na mbwa, lakini mbwa mwenyewe umemshikilia mnyororo, sasa mbwa atakamataje mwizi?
 
Chama ni chao, na serikali ni yao, lakini bunge si lao. Na spika si wao. Makamba hajui maana ya demokrasia na usimamiaji wake. Amezoea ubabe ubabe tu. Ndo mananga waliopo CCM hawa.

Salute.

na unapokuwa una-ongozwa na viongozi wa aina hii at least ndani ya chama, tukuite una akili timamu au?
 
Makamba kasema hiviiii!

CHAMA NI CHETU, SERIKALI NI YETU, BUNGE LETU, NA SPIKA NI WETU.

Bandugu, huyu mzee ana-akili timamu?

yeah, niliuliza huko nyuma kuwa je kumbe serikali na Bunge siyo mali ya wananchi bali ni vya CCM? Kwa hiyo ndiyo maana wanafanya maamuzi ambayo hayajali interest za nchi.
 
Teh teh Teh teh Teh teh Teh teh,
alisahau kutaja na ufisadi, kuvunja katiba, wizi wa kura, ubabe na kutokuwa na demokrasia ni vya chama chao
 
Salute.

na unapokuwa una-ongozwa na viongozi wa aina hii at least ndani ya chama, tukuite una akili timamu au?

mh si ndo hapo!! Kuongozwa nao = kuwakubali
kuwakubali = kuwasupport
kuwasupport = ?????
 
makamba????????!!!!!!!!!

kauli zake ni za ajabu ajabu kama rangi ya kinyonga...

ndio maana alipewa ubunge wa kuteuliwa maana mteuwaji alishajua madudu yake yakiwemo hayo ya kubwatuka bwatuka bila kufanya tathmini ya hao wanaopewa au kufikishiwa ujumbe.

Inafaa ubunge wa kuteuliwa uondolewe na akina makamba waende nao dimbani ili tujue uwezo wao kujieleza au kusema points ili kukitetea chama kwa hoja na kuzitangaza sera za ccm...
 
Mliyataka wenyewe, nakubaliana na kauli ya Makamba. huyu sio mtu wa kwanza kwa kutamka maneno hayo, kumbuka Sumaye alipokuwa waziri mkuu akihutubia Moshi alisema hivi "Ukitaka kufanya bihashara isiyokuwa na usumbufu na kusumbuliwa na TRA hakikisha unakuwa mwana CCM!! Kuna tofauti gani na kauli ya Makamba? Hapa maana yake kila kitu wanao uwezo wa Ku-Dictate!! Mpo.

Ushauri wa kukomesha manano ya jeuri kama haya ni Through "ballot Box"
 
Back
Top Bottom