Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Kama mtakumbuka, mwaka 2019 nilienda Ulaya nchini Ujerumani katika viwanja vya Bayern Munich (Alianz Arena) na ule wa Dortmund (Signal Iduna Park) kujifunza namna ya kuboresha viwanja vya soka.
Faida niliyopata kule ni ndo haya Mapinduzi mnayoyaona hapa kwenye uwanja wetu.
Msimu uliopita tuliweka nyasi bandia namba moja duniani kwa sasa.
Msimu huu pia tunakuja na vitu namba moja.
Leo tunaanza kuweka taa za kisasa za LED kama zilizopo kwenye viwanja vikubwa vya Ulaya.
Hizi ni taa zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ambayo inaweza kutusaidia kuweka rangi tofauti tofauti uwanjani.
Yaani pale katikati kwenye dimba tunaweza kuweka maandishi tunayoyataka, kwa mfano, Azam FC au tunaweza kuweka picha ya mchezaji aliyefunga bao na watu wanaotazama kwenye TV wakaona.
Pia tunafunga mabango ya kisasa ya matangazo pembeni ya uwanja.
Haya ni mabango yanayotumia umeme na yatasaidia kurusha matangazo mengi wakati wa mchezo badala ya kuwa na mabango yanayobeba tangazo moja kila siku.
Zoezi la uwekaji vitu hivi linaweza kuchukua wiki mbili hadi tatu.
Tukishamaliza hilo, tunahamia kwenye kufunga majukwaa.
Majukwaa tutakayoweka ni ya kisasa pia, ambayo siyo ya kujenga bali ya kufungwa kwa umeme.
Wakati wa mechi, unawasha swichi, yanakunjuka na watu wanakaa.
Mechi ikiisha, unazima swichi, yanajikunja na kuacha eneo la wazi kama hakukuwa na kitu.
Majukwaa haya yatasaidia kuficha maeneo ya wazi endapo hakutakuwa na mashabiki wengi uwanjani, badala ya kuonekana mapengo mengi.
Majukwaa tunayotaka kuweka yatakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 hadi 40,000.
Huu ni uwekezaji ambao wakurugenzi wameamua kuufanya kwa ajili ya klabu yetu na soka la Tanzania kwa ujumla.
- Injinia Victor Ndozero.
Mhandisi mkuu wa uwanja wa Azam Complex Chamazi