Chamazi itakuwa ya kisasa

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Kama mtakumbuka, mwaka 2019 nilienda Ulaya nchini Ujerumani katika viwanja vya Bayern Munich (Alianz Arena) na ule wa Dortmund (Signal Iduna Park) kujifunza namna ya kuboresha viwanja vya soka.

Faida niliyopata kule ni ndo haya Mapinduzi mnayoyaona hapa kwenye uwanja wetu.

Msimu uliopita tuliweka nyasi bandia namba moja duniani kwa sasa.

Msimu huu pia tunakuja na vitu namba moja.

Leo tunaanza kuweka taa za kisasa za LED kama zilizopo kwenye viwanja vikubwa vya Ulaya.

Hizi ni taa zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ambayo inaweza kutusaidia kuweka rangi tofauti tofauti uwanjani.

Yaani pale katikati kwenye dimba tunaweza kuweka maandishi tunayoyataka, kwa mfano, Azam FC au tunaweza kuweka picha ya mchezaji aliyefunga bao na watu wanaotazama kwenye TV wakaona.

Pia tunafunga mabango ya kisasa ya matangazo pembeni ya uwanja.

Haya ni mabango yanayotumia umeme na yatasaidia kurusha matangazo mengi wakati wa mchezo badala ya kuwa na mabango yanayobeba tangazo moja kila siku.

Zoezi la uwekaji vitu hivi linaweza kuchukua wiki mbili hadi tatu.

Tukishamaliza hilo, tunahamia kwenye kufunga majukwaa.

Majukwaa tutakayoweka ni ya kisasa pia, ambayo siyo ya kujenga bali ya kufungwa kwa umeme.

Wakati wa mechi, unawasha swichi, yanakunjuka na watu wanakaa.

Mechi ikiisha, unazima swichi, yanajikunja na kuacha eneo la wazi kama hakukuwa na kitu.

Majukwaa haya yatasaidia kuficha maeneo ya wazi endapo hakutakuwa na mashabiki wengi uwanjani, badala ya kuonekana mapengo mengi.

Majukwaa tunayotaka kuweka yatakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 hadi 40,000.

Huu ni uwekezaji ambao wakurugenzi wameamua kuufanya kwa ajili ya klabu yetu na soka la Tanzania kwa ujumla.

- Injinia Victor Ndozero.

Mhandisi mkuu wa uwanja wa Azam Complex Chamazi
 
Azam wanafanya mabadiliko ambayo kwa East Africa viwanja vingi hakuna.

Hii ni hatua nzuri sana kwa Azam kama football club na Tanzania pia, naamini kwa mabadiliko haya hiki kiwanja kinaweza pitishwa na FIFA kuwa kiwanja kinachokidhi ubora wa kimataifa.
 
Indeed.
Azam watafute namna pia ya kuifanya team iwe na sehemu ya wanchama na wapenzi,wajaribu kuifanya kuwa klabu ya watu ili kupata surport ya wanachama kwenye kushangilia/hamasa kwa team na mambo mengine.
U nailed it....tatizo kubwa la azam ni fan base.
 
Indeed.
Azam watafute namna pia ya kuifanya team iwe na sehemu ya wanchama na wapenzi,wajaribu kuifanya kuwa klabu ya watu ili kupata surport ya wanachama kwenye kushangilia/hamasa kwa team na mambo mengine.
U nailed it....tatizo kubwa la azam ni fan base.
Kwa nini wasiwashawishi kina maulidi wakawa wanachama maana naona sekta zao nyingi ndio wameajiriwa.
 
Bila kuweka nyasi halisi fifa hawapitishi kamwe
 
Kwa nini wasiwashawishi kina maulidi wakawa wanachama maana naona sekta zao nyingi ndio wameajiriwa.
Hapana waanze ushawishi kwa watoto na vijana wadogo,jitu kama Kitenge unalitoa kushabikia Yanga kwa kuanzia wapi kwa mfano.
 
Simba wao wametandika kapeti pale bunju,[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] kelele nyingi kuwahadaa mashabiki
Hizi timu zetu za Simba na Yanga ni blabla tu akuna cha maana.
Pale Yanga pakichaluka kuulizia uwanja wa Kigamboni umefikia wapi basi utaonyeshwa video ya mwaka jana greda likipaua uwanja"kisha utaambiwa kazi inaendelea site"
Ni aibu kwa klabu kongwe za Simba na Yanga kukosa viwanja vya maana kama wanachokarabati Azam f.c hivi sasa.
 
Dah, technolojia inakuwa kwa kasi sana,
huwa natazama yale majukwa kwenye music awards; mfano BET, Black Music Honours, Soul train au MTV Awards yanavyokuja na kupotea yaani ni amazing.... big up sana kwa Azam kwa hatua hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…