Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Mimi sio shabiki wa muziki wa kizazi kipya, iwe kutoka kwa Diamond, Ali Kiba au msanii mwingine yeyote wa rika lao, lakini kuna jambo limenivutia sana. Nikiwa ofisini, wadada wawili walikuwa wanakula karanga zilizoandikwa ‘Diamond Peanuts’, walizozinunua na kuzisifia kuwa ni nzuri sana. Sikuwatilia maanani nikichukulia kuwa ni mashabiki wa Diamond.
Haikuchukua muda mrefu, kituo cha redio cha Clouds wakawa wanapiga wimbo wa Diamond wa “Chambua kama Karanga”, aliokopi vionjo kwa Saida Karoli.
Sijui kwanini, lakini nikanijia wazo kuwa wimbo huo una uhusiano fulani na karanga za Diamond, jambo ambalo sikuwahi kulifikiria kabisa. Mwanzoni niliposikia watu wakiuzungumzia wimbo huo (sikuwa nikiufuatilia japo leo nimejikuta nausikiliza kwa makini) nilidhani alipendezwa tu na kibwagizo cha ‘chambua kama karanga’, na wengi wakasema amemuibua Saida Karoli kiaina.
Inawezekana wapo sahihi, maana baada ya wimbo huo, Saida Karoli amerudi kwa mshindo mkuu akiwa na vionjo vilevile kwa wimbo wake mpya wa “Olugambo” (kama sijakosea).
Ila nawaza: Wakati Diamond anaimba habari ya karanga, ni kweli alivutiwa na vionjo vya Saida Karoli, au ilikuwa ni mpango wa mbele wa kuzindua mradi wake wa Diamond Peanuts? Na kama ilikuwa ni mbinu ya kibiashara, basi aliona mbali sana.✔
Najaribu kuwaza kwa sauti…