Sasa dereva wa watalii unamtozaje leseni kwa dola!!?. Inamana serikali ndiyo inayohamasisha dollarazation. Huu ni ujinga mkubwa.
Ukweli ni kuwa dollar yoyote inayoingia nchini inatakiwa kuingia serikalini, na serikali impe yule anayetaka kutumia pesa humu ndani Tsh. Hakutakiwi kuwa na Buro de change yoyote wala kuchange dola hotelini wala mtaani. Benki za serikali ndizo zinatakiwa kupokea na kuchange dollar zote nchini. Dollar amazo mwishowe huingia hazina. Mfanyabiashara akitaka kununua kitu nje serikali ipokee Tsh zake na kumpa dollar akanunue vitu. Bila ya hivyo dollar itazidi kuadimika huku ikidhidi kuongezeka thamani.
Hivyo ndivyo serikali ya China ilivyoweza kutengeneza akiba ya dola. Lakini hii system inahitaji ukauzu sana kwenye usimamizi. Vinginevyo wahuni watakuwa wanajikombea akiba ya dollar zilizoingizwa nchini na wakulima wa mazao ya biashara, wachimba dhahabu na makampuni ya kitalii na kisha kwenda kuzitumbua. Mtu kama JPM pekee ndiye alikuwa anaelekea kusimamisha system kama hii.