Champions League last 16: Real Madrid kuivaa PSG; Chelsea kukipiga na Barcelona

Champions League last 16: Real Madrid kuivaa PSG; Chelsea kukipiga na Barcelona

Chelsea-squad-.jpg
Chelsea wamepangwa kukutana na Barcelona hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Tottenham nao wakapewa mabingwa wa Italia Juventus baada ya droo kufanywa.
Viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City watakutana na FC Basel ya Uswizi, Manchester United wakutana na Sevilla wanaocheza La Liga nao Liverpool wakutane na FC Porto ya Ureno.
Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Paris St-Germain.
Klabu tano kutoka England zilifuzu kwa hatua ya makundi msimu huu, ambayo ni rekodi.
Chelsea ndio pekee wa Uingereza waliofuzu wakiwa wa pili kutoka kundi lao, klabu nyingine zote zilimaliza kileleni.
Washindi wa makundi watakuwa ugenini mechi za kwanza 13/14 na 20/21 Februari na nyumbani mechi za marudiano mbamo 6/7 na 13/14 Machi.
Fainali itachezewa Kiev mnamo 26 Mei.
Droo kamili: Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Juventus Tottenham

FC Basel Manchester City

Sevilla Manchester United

Real Madrid PSG

Shakhtar Donetsk AS Roma

Chelsea Barcelona

Bayern Munich Besiktas

FC Porto Liverpool

SOURCE: TANZANIAONE BLOG
 
WAtu ni wepesi sana kusahau EPL pale hamna kitu hasa zikifika hatua kama hii.. Team ya pekee yenye nafasi kubwa ni Man City zilizobaki kutoka EPL nafasi ya kutolewa ni kubwa mnoo.. Porto atamuabisha Liverpool.. Na kwa hii Chelsea ni ngumu mno kumtoa Barca.. Man U naye haeleweki kabisa Seville atampa kibano. Juve licha ya kiwango kutokuwa sawa ila uzoefu utambeba sana dhidi ya Totenham
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom