Chande's commission of inquiry used, misused, abused, and now confused

Chande's commission of inquiry used, misused, abused, and now confused

Izato

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
5,441
Reaction score
11,669
Tume ya Chande iliteuliwa na watawala ikiwa na malemgo ya
  • Kupata ukweli wa nini kilitokea? Nani alihusika? Na kwa nini ilitokea hivyo?
  • Kuwajibisha ikiwa kuna mtu alikiuka sheria au maadili
  • Kutoa mapendekezo ili kuweza kuzuia jambo hilo lisitokee tena.
Lakini jambo kubwa la kushangaza ni pale malengo ya tume yalipodhibitika kudogoshwa kwa makusudi ili kuweza kuwasafisha watawala kutokana na kadhia zilizotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Octoba, 29 mwaka 2025 hali iliyopelekea maandamano, mauaji ya halaiki, na uharibifu wa mali.

Kwa muktadha huo basi yafuatayo yaliweza kubainika kuhusiana na tume hii,

1. Used - Kutumika
Mtawala amefaidika na tume kwa sababu imekuwa na thamani kwake, lakini si kwa sababu ya maslahi mapana ya Taifa letu.

2. Misused - kutumiwa visivyo
Tume iliikosa uhuru, na mipaka ya mamlaka yake iliingiliwa na watawala kwa makusudi au kwa uzembe.
Watawala waltoa hadidu za rejea kwa tume huku wakijua matokeo yake yatakuwa na manufaa kwao.

3. Abused - Kudhalilishwa
Mipaka ya mamlaka ya tume ilivunjwa ili kuweza kudhibitiwa na watawala. Weledi wa wajumbe wa tume ulidogoshwa huku wakllazimika kukubaliana na hali hiyo kwani waliona bayana hawana nguvu ama uthubiutu wa kusema hapana ama kwenda kinyume na matakwa ya mtawala

4. Confused - Kuchanganyikiwa
Baada ya kukabidhi ripoti yao kwa mtawala, huku ikikabiliwa na ukosolewaji mkubwa kutokana na hotuba yao waliyoitoa kwa umma, tume haijitambui tena. Hajui kilicho cha kweli, kilicho cha uongo, kilicho kizuri, ama kilicho kibaya.
Mtawala kaipoka ripoti ya tume na kusema ni mali yake mwenyewe huku tume imebakia
inajitetea mbele ya umma kwa kuwa,
  • Mtawala ameshafaidika kwa kuigeuza tume kama toilet tissue
  • Tume inahisi kila kitu kimetokana na kosa lao
  • Wajumbe wabobezi na wabobevu wa tume wanashindwa kuamini kwa akili zao wenyewe kwa yale yanayowatokea

Hitimisho
What comes around, also goes around.
 
Back
Top Bottom