Changamoto baada ya kuweka tiles(vigae)

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Kuna madoa ya wakati wa ujenzi nayo ni hatari ,ukipata fundi sio msafi wakati wa kuweka tiles ataacha alama kila kona .
Madoa,kwa mafundi wa mtaani ni changamoto,sio wasafi kabisa
 
Hao wa vijana wa mtaani wengi sio watalaamu ,Mother hopo ni kwake ndio aliwaleta yeye anaona sawa ila wamechafua ...Bado wa rangi nao ukutani wamechafu yaani tafarani.
 
Kwahiyo mkuu kwa uzoefu wako hayo maji yanaweza kuwa shida ni nini
 
Inaonekana ulijenga eneo oevu(lenye maji) bila kuchukua tahadhali kwa kulaza nylon na kumwaga oversite concrete.

Kwahiyo kufanya maji yatoke chini na kupanda juu.

Kama hautafanya marekebisho kwa kufumua hizo tiles na kufanya hicho cha juu basi tiles zenyewe zitatoka zenyewe hapo baadaye.

Pole sana
 
Tiles zilizotumika ni kampuni/trade name gani kwanza?
Nahisi ndio zenye shida ya kuyeyusha material fulani yaliyo chini yake inaponyesha mvua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…