Changamoto baada ya kuweka tiles(vigae)

Changamoto baada ya kuweka tiles(vigae)

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Wataalamu wa ujenzi, nimeweka tiles nyumbani kwangu,lakini baada ya miezi miwili kupita vinatokea hivi vitu.

Ni kama maji lakini ni mazito kiasi yanavutika,yakikauka yanaacha rangi nyeupe,hata ukisafisha hayatoki kirahisi,yakitoka baada ya muda yanatoka tena.

Je shida inaweza kuwa ni nini.
Nb.Nyumba imepigwa jamvi,lakini dpm haijawekwa.

Picha zinajielezaView attachment 2831393View attachment 2831394View attachment 2831395View attachment 2831396View attachment 2831397View attachment 2831398
20231202_131650.jpg
 
Kuna madoa ya wakati wa ujenzi nayo ni hatari ,ukipata fundi sio msafi wakati wa kuweka tiles ataacha alama kila kona .
Madoa,kwa mafundi wa mtaani ni changamoto,sio wasafi kabisa
 
Hawa ni mafundisho wa wapi washamba hivi mpaka Sasa hivi wanaacha space kati ya kigae? Huo ni uchafu uliopindukia kwani wataalamu wa Sasa hivi hawatumii tena ma spacer na vigae vinakuwa na mwonekano mzuri na hakuna tatizo sijui lanupumuaji, sijue kutanuka hakuna
Hao wa vijana wa mtaani wengi sio watalaamu ,Mother hopo ni kwake ndio aliwaleta yeye anaona sawa ila wamechafua ...Bado wa rangi nao ukutani wamechafu yaani tafarani.
 
Hawa ni mafundisho wa wapi washamba hivi mpaka Sasa hivi wanaacha space kati ya kigae? Huo ni uchafu uliopindukia kwani wataalamu wa Sasa hivi hawatumii tena ma spacer na vigae vinakuwa na mwonekano mzuri na hakuna tatizo sijui lanupumuaji, sijue kutanuka hakuna
Kwahiyo mkuu kwa uzoefu wako hayo maji yanaweza kuwa shida ni nini
20231202_131739.jpg
 
Inaonekana ulijenga eneo oevu(lenye maji) bila kuchukua tahadhali kwa kulaza nylon na kumwaga oversite concrete.

Kwahiyo kufanya maji yatoke chini na kupanda juu.

Kama hautafanya marekebisho kwa kufumua hizo tiles na kufanya hicho cha juu basi tiles zenyewe zitatoka zenyewe hapo baadaye.

Pole sana
 
Tiles zilizotumika ni kampuni/trade name gani kwanza?
Nahisi ndio zenye shida ya kuyeyusha material fulani yaliyo chini yake inaponyesha mvua
 
Back
Top Bottom