Changamoto baada ya kuweka tiles(vigae)

Kuna uwezekano kwenye msingi kukawa na bomba limepita (linavuja) au water table ya hilo eneo ipo juu. Huyo fundi hukumnunulia grout? Mbona kama ameunga tiles kwa kutumia cement.
Grauti zilinunuliwa za kutosha mpka nyingine zilibaki,hiko eneo water table ipo juu kweli,ila jengo lilipigwa jamvi kabla ya kuweka tiles, kitu ambacho nimeona ni kwamba hizo sehemu ambazo huo uchafu unatoka kuna nafasi ambazo grout haijawekwa!, hayo maji sio kama maji ya kawaida mana ni kama chemical reaction mana ni mazito na yanavutika yakikauka yanaacha rangi nyeupe,najiuliza yanatokea wapi sipati jibu
 
Hiyo rangi nyeupe inayoachwa baada ya maji kukauka kwa asilimia kubwa inaweza ikawa ni chumvi au kitu chenye tabia inayofanana na chumvi, ukichukua maji yenye chumvi ukaweka mahali penye jua, maji yataondoka chumvi itabaki. Ungekuwa umeweka lile nylon kabla ya kumwaga jamvi, hiyo shida usingeiona
 
Ardhi ya eneo umegenga nyumba ikoje!?
Ina maji maji,lakini kabla ya hapo palikuwa na nyumba nyingine,uliwekwa sakafu ya cement hakukuwa na changamoto kama hii
 
Asante mkuu kwa mawazo yako
 
Tiles zilizotumika ni kampuni/trade name gani kwanza?
Nahisi ndio zenye shida ya kuyeyusha material fulani yaliyo chini yake inaponyesha mvua
Grauti zilinunuliwa za kutosha mpka nyingine zilibaki,hiko eneo water table ipo juu kweli,ila jengo lilipigwa jamvi kabla ya kuweka tiles, kitu ambacho nimeona ni kwamba hizo sehemu ambazo huo uchafu unatoka kuna nafasi ambazo grout haijawekwa!, hayo maji sio kama maji ya kawaida mana ni kama chemical reaction mana ni mazito na yanavutika yakikauka yanaacha rangi nyeupe,najiuliza yanatokea wapi sipati jibu
 
Asante sana mkuu
 
Ina maji maji,lakini kabla ya hapo palikuwa na nyumba nyingine,uliwekwa sakafu ya cement hakukuwa na changamoto kama hii
Hizo tiles hazikuwekwa na fundi professional...! Nimegundua hilo baada ya picha moja kuonesha tofauti kubwa ya lines!
Pia hata uwe Groute, ama hawakutumia Groute yenye
Ubora ama hawakuweka kwa Utaalam!

Kwa sababu Groute ina cement na mchanganyiko mwingine ndani yake, uki apply vile inatakiwa, haiwezi kuruhusu maji mazito kama hayo kutoka ndani kuja nje, zaidi ungeona Groute ina unyevu tu.

Ndo mara ya kwanza kuona kitu kama hicho.
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…