Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 73,773
- 102,126
Ujue namimi najiuliza kama wewe, haya mambo yanaendaje? Ndiyo maana nikakuuliza ingekuwa ni wewe ungemuacha mtoto wako mazima kwa mwanaume mwingine? I wish tungepata ka-testimony
Paragraph ya mwisho imeniwazisha mweeh. Imagine baba mzazi ana ndoto za mtoto wake asome Feza labda, afu mama alipoolewa kule baba uwezo wake ni St Mary's maybe; ndiyo yale kila mtoto atakwenda shule kutokana na uwezo wa baba yake au? Mind you yule ni mtoto wake, ana ndoto juu ya mtoto wake na ana uwezo wa kuzitimiza; je azikatishe na kukaa chonjo kisa mtoto anaishi kwenye paa ya mwanaume mwingine? (Naongelea kwenye situation ambazo maybe ni salama zaidi mtoto kukaa na mama, imeshindikana kukaa na baba). Au kwa single mom with multiple baby daddies, na kila baba anahudumia mtoto wake kwa uwezo wake.
Mtazamo wangu upo hivi kulingana na scenarios tofauti tofauti, sijui kwa wengine...
1. Nikiamua kuoa mwanamke ambaye ni single mom, basi hata mwanaye/wanaye watakuwa chini ya himaya yangu kwa kila kitu...
2. Endapo mimi ni mwanaume niliyemzalisha mwanamke na mwanamama huyo akaolewa na mwanaume mwingine, nitamfungulia mtoto akaunti na hela yake nitaweka huko. Akiwa mkubwa atakutana nayo...