Mustafa James
New Member
- May 22, 2024
- 2
- 0
Katika jamii ya watanzania kuna makundi mbalimbali ya watu wenye mahitaji mbalimbali yanayotofautiana, hata hivyo zipo njia mbalimbali za kuwafikishia mahitaji watu hao katika makundi yao.
Makundi ya walemavu wamekuwa wahanga wa kutopata huduma sitahiki katika jamii kwa maana ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Kuna aina kuu sita za makundi ya walemavu dunianj kote ambapo hata hapa Tanzania makundi hayo yapo. Makundi hayo ni kama; wenye ulemavu wa viungo, wasioona, walemavu wa akili, viziwi,viziwi wasioona na wenye uarubino. Kumekuwa na changamoto nyingi sana kwa makundi haya ya walemavu ambazo zimekuwa zikiathiri moja kwa moja maisha yao na kupelekea uduni na udhaifu mpaka mwisho wa maisha yao.
Zifuatazo ni changamoto zinawakumba makundi ya walemavu ambazo hazijapatiwi usaidizi au ufumbuzi na serikali
1. Elimu duni kwa walemavu nchini ambapo mpaka sasa kuna vituo vinavyoweza kutoa elimu kwa walemavu wa aina mbalimbali 806 tu nchini huu ni upungufu mkubwa sana ukilinganisha na mahitaji ambapo angalau kila kijiji au mtaa panahitaji uwepo wa kituo au shule hata hivyo hata mtaala wa elimu ya tanzania umetaja tu lugha za walemavu ila hautaji mbinu za kufundshia walemavu yaani mtu analazimika kutumia mbinu za wpkufundishia wanafunzi ambao hawana ulemavu kufundishia wanafunzi wenye ulemavu kwa mfano kitabu cha kiada utakuta kimeandikwa kuimba wimbo kwa sauti maana yake hapa mlemavu kiziwi hajajumuishwa katika mbinu hiyo.
2. Kukosekana kwa wakalimani wa lugha ya alama katika vikao, na mikutano ya hadhara inayolenga kuelimisha au kutoa taarifa juu ya jambo fulani katika jamii jambi hili limepelekea walemavu wengi kutengwa katika shughuli za maendeleo kwani hawapati taarifa hata ya mambo madogo ya kawaida na kupelekea kuonekana kama watu wasiokuwa na maana kwenye jamii.
3. Kukosekana kwa wakalimani wa lugha ya alama na wataamu wa nukta nundu hospitalini na votuo vya polisi hali hii imepelekea walemavu hasa wa uoni na uziwi kutoenda kutafuta matibabu hospitalini kwa kuhofia kutoeleweka maelezo yao na hata vituo vya polisi wanapotendewa unyanyapaa au kuonewa kwa namna yoyote.
4. Vyama vya siasa vingi vinawabagua walemavu wa uziwi na uoni katika kugombea nafasi pale wanapohitaji kwa kuona kama hawataweza kumudu kusimamia majukumu wanayopaswa kusimamia licha ya wao wenye kuwa na uwezo huo.
5. Ukosefu wa vituo tosherezi vya kutunzia walemavu wa akili na wenye mtindio wa ubongo hali hii imepelekea walemavu wengi wa akili kuonekana mtaani bila usaidizi wowote jambo ambalo ni aibu kwa nchi na fedheha.
6. Walemavu wa viungo wengi hawana vitimwendo jambo linalokwamisha wao kutekeleza majukumu yao kama watu wengine na hali ile huwatia katika umasikini mkubwa na kuishia kuwa ombaomba watu walio karibu yao.
Mambo yafuatayo yafanyike ili kutengeneza usawa katika jamii kwa kuwawezesha walemavu kuwa sawa na watu wengine nchini Tanzania.
1. Kika mtaa au kijiji kiwe na uwezo mfumo wa kuwatambua walemavu tangu wakiwa wadogo na kutengeneza mazingira ya kuwaanzisha shule katika mtaa au kijiji walipo na sio kuwapeleka shule za walemavu za mbali kwani jambo hilo hupelekea wazazi wengi kushindwa na kuamua kutowasomesha walemavu kwa kukwepa gharama.
2. Mtaala wa elimu uwe wazi kwa wanafunzi kwa maana ya mitihani ya walemavu iendane na mahitaji yao mfano viziwi wasifanye mtihani wa wanafunzi ambao sio viziwi kutokana na utafauti walio nao katika kupokea taarifa
Muda wa kuhitimu elimu ya msingi kwa viziwi uwe sawa Tanzani nzima kwa kuwa shule nyingine hutumia miaka 10 kwa viziwi nyingine miaka 7.
3. Lugha ya alama ifundishwe kama somo kwa wanafunzi wote kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu ili kurahisisha mawasiliano kwa viziwi pote nchini. Hii iendane na ufundishaji wa nukta nundu za wasioona.
4. Taasisi za kisiasa ziwaamini walemavu kwani wanaweza na ni wazalendo sana kwa taifa lao. Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya wajenge vituo tosherezi nchi vya kuwatunzia watu wenye ulemavu n magonjwa ya akili ili kuepusha watu hao kubaki mtaani. Na kuzurura mwisho kuishi kama wanyama.
5. Serikali ichukue hatua za makusudi kusomesha wataalamu wa kutosha watakao hudumia walemavu katika vitengo tofauti hasa katika kipengele cha kutoa na kupokea taarifa kwa sababu mpaka sasa walemavu wengi wako gizani
Ni mimi Mustafa James Katole
0782593170

Upvote
2