KERO Changamoto katika utoaji huduma ofisi za Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

KERO Changamoto katika utoaji huduma ofisi za Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Utoaji huduma kwa jamii unatakiwa kuwa rafiki ili kufikia malengo yaliyowekwa kwa manufaa ya TAIFA letu.
Mimi kama mchangiaji wa NHIF kuna changamoto nimeziona katika ofisi za NHIF (Chache kama sio zote).

1. Utashi mdogo kwa baadhi ya watoa huduma.

Mteja anapohitaji kujisajili/kuendelea na huduma katika utoaji wa maelekezo watoa huduma hukinzana katika viambatisho. Uliyemkuta juzi atakupatia maelekezo tofauti na uliyemkuta jana. Kwani ofisi hazina miongozo ili mtoa huduma awe anapiga chabo kama kichwa hakiko vizuri?

Mteja anajaza fomu anaziwasilisha anapatiwa ankara ya malipo analipia halafu viambatisho vikimfikia mtoa huduma mwingine zinaonekana hazijakamilika.

Kwanini muidhinishe malipo wakati viambata havijakamilika?

2. Lugha mbovu ya mawasiliano

Mara zote tunaamini mtoa huduma wa Sekta husika anakuwa na uelewa wa jambo analolitolea huduma, hivyo kutakiwa kutoa maelezo kwa lugha stahiki isiyo na mihemko.
Cha kushangaza imekuwa tofauti kwa watoa huduma wetu, wanaongea kama wamekurupushwa na mihemko juu.

3. Urejeshaji wa kadi za bima

Hapa ni kwa uongozi wa Shirika, mnatakiwa kuiga kama wafanyavyo benki katika urejeshaji wa kadi zilizopotea/kuharibika.

Tuko Ulimwengu wa digitali, kwanini kujaza jaza mikaratasi maofisini wakati taarifa za mwanachama zinaonekana kwenye mfumo?

Kama kadi imepotea ama kuharibika ina maana mwanachama alipatiwa kadi kwa kutimiza vigezo vyote, iweje muanze kurundika sijui vyeti vya kuzaliwa, taarifa ya upotevu. Yote hayo ya kazi gani? Kwanini kusiwe na Taarifa ya upotevu tu ili mhakiki taarifa za mteja wenu kupitia namba ya uchangiaji?

Haya yamebainika tawi la ILALA, bila shaka yatakuwa yanafanyika karibu ofisi zote.

Ni KERO kubwa kwa watumia huduma. Mjirekebishe.
 
Kibaha ndio Kuna hizo changamoto. Nashangaa nchi hii inawasomi kibao jobless, chakushangaza NHIF wanaajiri watu mbumbumbu.
Ukifika NHIF Ni Kama umefika kituo Cha polisi wa Burundi. MTU unakwenda kuwalipa pesa lkn wanakuona Kama mtuhumiwa fulani.
 
Kibaha ndio Kuna hizo changamoto. Nashangaa nchi hii inawasomi kibao jobless, chakushangaza NHIF wanaajiri watu mbumbumbu.
Ukifika NHIF Ni Kama umefika kituo Cha polisi wa Burundi. MTU unakwenda kuwalipa pesa lkn wanakuona Kama mtuhumiwa fulani.
Karibu ofisi za umma zote mimi huwa naona waliopo ofisini ndo wapuuzi kabisa heri ya waliopo mtaani, wahudumu wapo kama maroboti hawatumii akili kabisa
 
Katika ofisi za umma ukitaka kumuona mkurugenzi au kamishna au hata Hawa wa chini utaambiwa usubiri Sana eti mkubwa Yuko bize. Ripoti ya CAG ikitoka yule yule aliyejifanya Yuko bize idara yake au shirika limetia hasara ya mabilioni. Sasa unajiuliza, huyu kibaka alikua bize ana chati na kuangalia porn au alikua anatongoza wafanyakazi walio chini yake?
Sasa hivi NHIF ime collapse kwasababu ya uzembe wa watendaji, PSSSF ilikua nayo ifukiwe ikaokolewa na kikokotoo. Mawaziri wapo, makatibu wakuu wapo bize, wakurugenzi wapo, Wote Hawa mioyoni mwao wanasema WHO CARES! !!!!
hawana nyapara au hata kiherehere.
 
Back
Top Bottom