Changamoto kubwa kwenye mfumo mbolea za ruzuku

Changamoto kubwa kwenye mfumo mbolea za ruzuku

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Msimu wa kilimo 2022/2023, serikali imekuja na mfumo wa mbolea za ruzuku, ambapo mkulima ni lazima ajisajili kwenye madaftari ya wakulima yaliyosambazwa kote vijijini.

Changamoto kubwa iliyojitokeza ni wakulima wengi kutopata namba ambayo wanatakiwa kwenda nayo kwa wakala ili wakamilishe malipo na kuchukua mbolea.

Hadi sasa ni wakulima wachache sana walioweza kupatiwa namba hizo kwa sababu mfumo haufanyi kazi na wakulima wamejikuta njia panda. Watu wengi wanahitaji kununua mbolea lakini changamoto ni upatikanaji wa namba.

Haieleweki nini hatima ya hizi mbolea. Mbaya zaidi mawakala hawaruhusiwi kuuza mbolea kwa njia ya kawaida ukigundulika unafutiwa leseni ya biashara.

Naishauri serikali chini ya wizara ya kilimo ishughulikie hii changamoto haraka kabla ya msimu wa kilimo kuchanganya,vinginevyo itasababisha mtafuruku mkubwa.

Pia Mawakala wanalalamika kutolipwa fedha licha ya kuuza mbolea kwa ruzuku. Baadhi yao wameanza kugoma kuendelea na hili zoezi.

Tafadhari Moderator naomba huu uzi uache kwenye hili jukwaa ili ujumbe ufike kwa urahisi kwa wahusika.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom