Changamoto kwa Asasi za Kiraia (CSOs) katika upatikananji wa Ruzuku

Changamoto kwa Asasi za Kiraia (CSOs) katika upatikananji wa Ruzuku

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252
1584624412680.png

Asasi za Kiraia (CSOs) ni wadau wakubwa katika maendeleo kwa nyanja zote; kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na hata ki-teknolojia. Wafadhili (donors) hutumia Asasi za Kirai kama njia (channel) katika uwekezaji wa rasilimali fedha (investment) Bahati mbaya sana, Asasi nyingi hazina ufahamu namna ambavyo hawa wafadhili hufanya maamuzi (decision making) katika utoaji wa ruzuku. Kutokuwa na ufahamu juu ya mchakato kumezifanya Asasi nyingi kufanya makosa katika uombaji wa hizi ruzuku na matokeo yake, waombaji wengi hukosa fedha.

CHANGAMOTO KATIKA UOMBAJI WA RUZUKU.
Kuna aina 5 za changamoto ambazo Asasi za Kiraia hukutana nazo katika mchakato wa kuomba ruzuku kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, na changamoto hizi, kwa muda mrefu zimekuwa kikwazo kwa asasi nyingi kupata hizo ruzuku. Changamoto hizo ni

1. Kutotambua uwiano wa ruzuku na hadhi (status), ukubwa (size) na lengo la kuundwa kwa Taasisi (organization mission): Wafadhili wengi wanapotoa ruzuku, huainisha sifa ambazo muombaji (Taasisi) anapaswa kuwa nazo. Mara nyingi sifa hizi huwa ni; Taasisi kuwa imesajiliwa, Taasisi kuwa na uzoefu fulani katika usimamiaji wa miradi (NOTE: Hapa si wafadhili wote wanataka Taasisi zenye uzoefu), Taasisi kutokea katika eneo maalum n.k Bahati iliyo mbaya, Taasisi nyingi hutuma maandiko kwa wafadhili pasina kuangalia na kuzingatia uwiano huu, na hatimae hujikuta wanatolewa nje ya mchakato.

2. Kushindwa kuunda ubia madhubuti (strong partinership): Wafadhili wengi sasa hutaka miradi kutekelezwa kwa ubia miongoni mwa Asasi za Kiraia. Lengo la kutoa ruzuku kwa sharti la ubia ni kurahisisha utekelezaji wa mradi lakini pia kuleta ufanisi. Tatizo kubwa kwa Asasi za kirai ima hushindwa kabisa kutengeneza ubia kwa ajili ya utekelezaji wa mradi au kutengeneza ubia na Asasi isiyokidhi vigezo, na hatimae kutolewa katika mchakato wa uombaji wa ruzuku.

3. Kuandaa maandiko yasiyokidhi viwango (standards meeting project proposals) Mfadhili anapotoa wito kwa ajili ya uwasilishaji wa maandiko (Call for Proposals); huainisha muundo na muongozo ambao unapaswa kutumika katika uandaaji wa andiko. Kuandaa andiko kinyume na muongozo pamoja na muundo uliotolewa humfanya muombaji kutolewa katika mchakato wa uombaji wa ruzuku.

4. Kutozingatia ushindani katika uombaji wa ruzuku. Kwa sasa utoaji wa ruzuku umegubikwa na ushindani wa hali ya juu. Waombaji wa ruzuku wamekuwa ni wengi, lakini fedha zinazotolewa ni chache. Mfadhili anapopokea maandiko huyafanyia tathmini (evaluation) ambayo hujumuisha "technical evaluation" na "compliance checking". Ili kuhimili mkiki wa ushindani ni vyema muombaji akahakikisha anaandaa andiko bora pia kukidhi mahitaji yote yanayotakiwa (requirements).

5.Ujuzi katika usimamiaji wa Miradi. Hakuna mfadhili aliye tayari kutoa fedha yake kwa Taasisi ambayo haina ujuzi katika usimamiaji wa miradi. Na ili kujiridhisha; kabla ya fedha kutolewa; hufanyika tathmini juu ya uwezo wa Taasisi. Hapa lengo ni kuhakikisah fedha inaenda kwa Taasisi yenye uwezo wa kuisimamia mradi ili ilete matokeo tarajiwa; kwa sababu hata mfadhili nae hufanyiwa tahmini (evaluation) juu fedha atakazotoa kwa Asasi za Kiraia.
NOTE: Si wafadhili wote hutoa TU fedha kwa Asasi zenye uzoefu; kuna ruzuku za kiwango cha chini (small grants); hizi haziitaji sana uzoefu wa Taasisi katika utekelezaji wa miradi.


The Consult: +255 719 518 367
E-mail: theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam
Home of Project Management, Strategic Management and Fundraising Management.
SERVICE: Consultancy, Trainings and Proposal Write Ups
 
Back
Top Bottom