Changamoto kwa Waandishi wa Habari: (Mwandosya & Mwakyembe Kuundiwa Mzengwe)

Kigarama na wewe unazungumza kama unazijua siasa za Mbeya. Kwenye hiyo habari ukiondoa hilo suala la UNEC ni kitu gani kingine ambacho kina makosa, hakiwezekani kabisa, au ni cha kutunga na uzushi?

Jana nilikuwa mbeya na leo nilipolisoma Raia mwema nikaona kama vile wanasimuliwa yale niliyosimuliwa mbeya. kwa hakika wana mbeya ambao wanapigana kufa na kupona kuona watoto wao Mwandosya na Mwakyembe wanainuka kwenye siasa za tanzania wanapambana vikali na wanamtandao wa kikwete.

na kwa mfano wanasema waziwazi kwamba kama CCM ikiendelea kuwachokonoa mwandosya na Mwakyembe basi wao wako radhi mwaka 2010 kuiangusha CCM Mbeya Mjini kuliko kumpa Tom Mwang'onda ubunge!
 
wengine walioko huko ambao Rhoda anakwenda kuungana nao kwenye vita hivyo ni Luciano Mbosa katibu wa CCM Mbozi,Zakaria George (Bajoji)Mbarari,Tecla Mung'ong,o (Mpwa wake Mangula)Leonidas gama na wengineo wengi!
 

Kigarama,

Kama ungesoma yote yaliyioandikwa hapo juu ungepata majibu yote ya uliyoyandika hapo juu.

Ni uongo kwamba Mwakyembe ni mjumbe wa NEC.

Ni uongo kwamba Mwandosya ameanza kampeni ya urais 2010.

Ni uongo kwamba Mulla alitaka kutoa tamko la kumlaani Prof.

Ni uongo kwamba kikao kijacho kitawajadili Mwakyembe na Mwandosya.

Hayo mengine yote aliyoandika amerudia mambo ambayo yako wazi na yalishandikwa. Hapo hakuna habari mpya zaidi ya uzushi.

Kinachotokea Mbeya ni siasa za mkoa na sasa watu wanataka kuzipeleka zionekana kama za kitaifa.

Ukiangalia vita kubwa ni jimbo la Mbeya mjini ambalo sio la prof. wala la Mwakyembe. Wapambe wanakuza mambo na waandishi wanayabeba bila hata kufanya uchunguzi kidogo.

Sijaona juhudi yoyote ya kumhujumu Prof. Mwandosya au Mwakyembe ambazo ni co-ordinated kitaifa tokea kwisha kwa uchaguzi wa NEC. Baada ya kwisha kwa uchaguzi wa NEC, prof. amekaa kimya. Haya ya kuanza kumwandama kwamba anataka kugombea urais ni uwongo mtupu.

Nilishaandika siku nyingi kwamba Mwang'oda alifanya judgement mbaya. Imejengwa hisia kwamba kwenda kwake Mbeya ni kumpinga Prof. Kwahiyo hata 2010 itakuwa ngumu sana kwake kushinda ubunge. Asingeligombea NEC na Prof mwaka jana, jimbo lile angelipata hasa baada ya mbunge wa sasa kuwa pale miaka 10.
 

Mtanzania hapa una argument nzuri na mhariri wa raia mwema is working on the issue ili kuweka hii story kwa uwazi zaidi.
 

Concise and clear.

Sina sababu ya kuwa na mashaka makubwa kwamba haya hayapo katika siasa za Mbeya.
 
Hivi ukiwa mbunge wa kuteuliwa na rais huruhusiwi kuzungumza?.....huyu Tom mbona kimya sana.......au mimi ndio nimepitwa na aliyoyafanya bungeni?.......duuh mada imegeuka kuwa "makundi ya watu wa kutoka Mbeya"

Back to mada
Tumejiridhisha (unless waje wenyewe hapa)kuwa waandishi wa habari wakati mwingine wanachemsha (sio nyakati zote)......na ninafahamu wako hapa wanasoma.......na iwe matarajio yetu kuona wanarekebisha hilo
 
huu ni uandishi duni na wakichochezi tu, kama hiyo mikakati ipo, watu wa mbeya wataidhibiti wenyewe maana wametuonyesha kwamba wana uhuru wa kuchagua wanayotaka. waandishi hatuna sikuhizi

Sijaona uandishi duni hapa, naweza kuiita fairly good investigative story. Tukiangalia mwenendo wa issue nzima hii utagundua kuwa kuna ukweli ndani yake, na kama hii thread itaendelea kuwepo kwa miaka miwili lazima tutaona ukweli wa mambo. Inaweza kutusaidia kuanza kuona which one will flourish evil or good. Kama unavyojua siasa sasa hivi zimekuwa hijacked na wafanyabiashara kama kina Mula/Dhandho Co and Sons Ltd, RA na wengine ambao wanajaribu kuwafukuza viongozi wetu wanaopinga wizi, i hope hii thread itakaa kwa muda mrefu, mtakuja sema 2009.
 
Hawa CCM ni watu wa ajabu bse ukijaribu kudeal na kipenzi cha watu utaishia kukosa mwana na mbeleko.
Mbeya CCM hawawezi tia mguu bila company ya hao watu sasa wakiwaletea fitina wataona majibu ya wananchi kwenye kura.
Am sure CCM inaanza kumeguka na sichelei kuquote msemo wa Kolimba ya kuwa CCM sasa haina Dira KILA mtu ni kapteni na nafanya atakalo.
Kwa mwendo huu CCM itakufa natural death
 

NAPENDA KUWAPA TAARIFA KUWA MWAKYEMBE NI MJUMBE WA NEC AMBAE ANAWAKILISHA NAFASI TANO ZA BUNGE,WAO HUWA WANACAGULIWA MARA BADA YA BUNGE KUAPISHWA.NAKUMBUKA KATIKA UCHAGUZI ULE WAGOMBEA WOTE WALIMCHAGUA EMANUEL NCHIMBI KUHESABU KURA ZAO NA MWAKYEMBE ALIONGOZA UCHAGUZI ULE AKIFATIWA NA MH MREMA.
 
TSJ hicho kinatoa elimu nzuri, wandashi ni lini mtalinda heshima yenu ktk jamii hii ya Kitanzania?
 
Hakuna kitu kama hicho, wajumbe wa NEC ya CCM ni kama hapa:

http://www.ccmtz.org/halmashaurikuu.html

NDIO PAMOJA NA KUNIPA SOURCE YAKO YA INFORMATION MIMI PIA NAKWAMBIA KUWA INA MAKOSA HIO WEBSITE YA CCM.NARUDIA HATA KWA DAU LA VISENTI BILIONI TATU,MIMI NAIJUA CCM,NAIJUA SANA...NCHIMBI EMANUEL NDIE ALIEHESABU KURA NA MSHINDI WA KWANZA ALIKUWA NI MWAKYEMBE,WA PILI NIMROD MKONO,WA TATU NI FELIX MREMA NA WA NNE NI FAIDA BAKARI WA TANO NIMEMSAHAU
 
Mtanzania,
Dr. Mwakyembe ni Mjumbe wa NEC ya CCM na anawakilisha nafasi kumi za wabunge. Hapo haupo sawa mzee! Unapokosoa jitahidi wewe mkosoaji uwe na habari sahihi. Sasa hii yaweza kuonesha maoni yako yote si sahihi. RaiaMwema ni gazeti lenye waandishi makini sana, haliwezi kufanya kosa unalosema. Unawajua RaiaMwema? John Bwire, Johnson Mbwambo, Jenerali Ulimwengu, Mbaraka Islam, Chirwa etc. Fact ya ujumbe wa NEC hawawezi kuikosea hata kidogo........
 
...hapendwi mtu mwanawane CCM kuchimbana mikwara si ndio zao wanatafuta jinsi ya kuwafunika watu lakini wana-mbeya wanajua tamu na chungu ya hii michezo michafu ya NAMBARI ONE!!! Mwl. Nyerere alisema ukionja nyama ya mtu hutaacha kamwe kuila..ndio hawa walishazoea kubonyezana kizenji sasa wanakimbizana....Bado tutasikia mengi story iko bomba tu mtu wangu
 

I love Jambo Forum! Talk about doing your research before you speak! I wish mawaziri wetu wangekuja hapa wakapewa semina elekezi hata bila kwenda Ngurdoto!
 

Kijana hapa umeua..hata kutaja majina manne kati ya matano unastahili benefit of doubt hata kama kuna akina Petro hapa ambao hawakukubali!
 

Zitto,

Nakubali hapo data zangu kuhusu NEC ya CCM hazikuwa sahihi. Nilifanya juhudi kubwa kuaangalia kabla ya kuandika ikiwa ni pamoja na kutembelea
website ya CCM pamoja na katiba yao.

Naomba msamaha kwa hilo, pamoja na kufanya uchunguzi kabla ya kuandika
lakini sikuweza kupata usahihi wa Dr. Mwakyembe kuwa mjumbe wa NEC. Hivyo kuendelea kuamini kwamba sio mjumbe wa NEC.

Mambo mengine yote bado msimamo wangu ni kama mwanzoni.

Najua Raiamwema ni gazeti makini lakini walichoandika kwenye hiyo habari sio sahihi zaidi ya kwenda na uvumi wa mtaani.
 
ok fine...tatizo ni Lowassa na wenzake(apson, Rostam and co) wanapanga mkakati kuwaangusha hawa wawili,maana waliaibika walivyoshindwa kumuangusha mwandosya NEC baada ya kutumia hela nyingi sana zaidi ya 1 million US (ili wampitishe Tom).

Sasa wanajipanga upya iliwajaribu kusimamisha hata wabunge wao wapya, maana wakina mwandosya na mwakyembe wanaungwa mkono na wabunge wote kutoka Mbeya isipokuwa wawili...(Tom - Kateuliwa, Kyendesa-viti maalum) ambao ni kambi ya Mwang'onda.

Mulla (na Mwakipesile -Mkuu wa mkoa na hata ma DC)naye ni kambi yamtandao ambaye anatumika kufanya vikao vya siri vya kuwazushia hawa wawili na wamewekwa hapo kwa mkakati ya kumuangusha Mwsandosya. Team zinajipanga pande zote kuondoa huu mtandao mbeya...


Hawa wanamtandao ni aibu kwa nchi yetu...mpaka leo Raisi hajaja kuona wananchi wake Mbeya, anatarajiwa kuja labda Mei aubaadaye....hii ni baada ya Miaka kama 2 na nusu. amefika marekani mara 6. Aje bwana tunataka tumuone na tumueleze matatizo ya maendeleo ya mkoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…