Mwanakijiji,
Nafikiri unajua garbage IN garbage OUT, ukijenga nyumba kwa foundation mbovu, nyumba nzima inakuwa mbovu. Hiyo makala imejengwa kwa foundation mbovu sana. Ukweli ulioko kwenye hiyo makala ni ule ambao tayari tunaujua na hakuna jipya hapo zaidi ya uzushi.
Kwanza hilo la kwamba Dr. Mwakyembe ni mjumbe wa NEC sio kweli.
Pili, nguvu ya Mwandosya kule Mbeya ni kubwa mno kiasi kwamba huyo Mwenyekiti hawezi hata siku moja kuandaa kwenye mkutano ajenda ya kumjadili prof. kwa kutumia vigezo vya mitaani. Huyo Mulla hana ubavu huo kabisa. Wanaweza kumjadili Prof. Kama kuna jambo kweli amelifanya lakini sio kwa
kutumia haya maneno ya mitaani. Kwa yeyote anayeijua Mbeya vizuri anajua hilo.
Tatu, prof. Mwandosya sio mjinga, ni mtu mwenye ueleo na ambaye anajua siasa za CCM na kikomo chake. Kama CCM waliweza kumtupa Malecela bila sababu za msingi, yeye prof. atakuwa na uwezo gani wa kupambana na rais aliyeko madarakani? Labda mwandishi angesema Prof. anataka kuhama chama lakini sio ndani ya CCM. Prof. kufanya hivyo itakuwa ni kujimaliza kisiasa
na sidhani kama yuko tayari kwa hilo.
Nne, toka uchaguzi wa NEC umeisha, prof. Mwandosya amekuwa kimya na kuweka nguvu yake kwenye uongozi wa nchi na sio siasa za ugomvi za Mbeya. Sijasikia hata mahali popote wakiandika Mwandosya anatembelea mkoa huu au wilaya hii. Sasa ataanza kampeni ofisi kwake au nyumbani kwake?
Ushauri wa bure ni kwa Wabunge kuacha kulialia na kuweka nguvu zote kwenye ku deliver kwenye majimbo yao. Magazeti yanaweza kukujenga lakini pia yanaweza kukubomoa.
Huyo Lowassa wanayemsema, kama ana nguvu si angejiokoa yeye asivuliwe kuwa PM?