Changamoto kwa wadau wa utalii -kagasheki waambie watanzania

Changamoto kwa wadau wa utalii -kagasheki waambie watanzania

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
482
Ndugu wadau wa Biashara ya Utalii,

napenda kuchukua fursa hii kuweka bayana changamoto ya ki-biashara isiyo na ushindani wa haki inayotukabili katika biashara ya utalii hapa nchini kwetu.

Kwamba, wakati kila mmoja wetu akipambana kufa na kupona kuweza kumudu ongezeko kubwa la gharama za uendeshaji wa biashara ya utalii ikiwemo ongezeko la hivi karibuni la ada mbalimbali za kuingiza wageni katika Hifadhi za Taifa, kuna wenzetu wanazidi kupewa misamaha mikubwa ya ada za kuingiza wageni katika Hifadhi mbalimbali za Taifa hapa nchini. Misamaha hii iantolewa kimya kimya na hufikia hadi asilimia 50 (50%) ya ada halisi. Je, sisi pia tunastahili kupewa fursa hii??? Hii ndiyo changamoto yetu kubwa!

Tunaweza kujadili changamoto hii kupitia vyama vyetu rasmi (TATO & KIATO) na kutoa kauli/msimamo wetu wa pamoja ambao mwisho wa siku utalenga kutoa ujumbe kwa serikali iwe wazi zaidi ili kila mmoja wetu awe na fursa sawa na ya haki katika kufaidi keki ya Taifa letu na katika kumudu soko la ushindani wa kibiashara badala ya kuwapa fursa hiyo watu/kampuni chache tu! Hii italisaidia taifa kuwa Taifa la uwazi zaidi, lenye kuwajibika kwa raia wake wote bila upendeleo na hivyo kufaidi tunu tuliyopewa (hususani rasilimali zetu zikiwemo Mbuga za Wanyama, Mlima Kilimanjaro, Madini, nk) na Mwenyezi Mungu kama wengine wanavyofaidi keki hii kubwa bila kuwaalika wengine!

Hapa naambatanisha kielelezo cha mada kuu hapo juu.
Kagasheki na Nyalandu tunaomba utuambie Watanzania dhamana ya kugawa Mali za Watanzania na huo ujasiri wenu mmeupata wapi
 

Attachments

  • Barua ya Waziri kwa mdau wa utalii.jpg
    Barua ya Waziri kwa mdau wa utalii.jpg
    45.5 KB · Views: 70
Mkuu najua umeumia sana. tatizo sio Leopard tours, tatizo hapo ni CCM. Vuta subira 2015 sio mbali, yana mwisho wake hayo.
 
Mkuu najua umeumia sana. tatizo sio Leopard tours, tatizo hapo ni CCM. Vuta subira 2015 sio mbali, yana mwisho wake hayo.

Yana mwisho upi mkuu wakati watu watakuwa wamesha sign mkataba wa miaka kibao?
 
Yana mwisho upi mkuu wakati watu watakuwa wamesha sign mkataba wa miaka kibao?

lazima vigezo havijafuatwa. Huyo jamaa anafahamika sana kwa kutoa rushwa. Fazal ni mtoa rushwa mzuri sana. yote hayo yatatizamwa upya by 2015, kwa sasa huwezi shindana nae. Kule netwest bank anzo pesa za kutosha. Subiria utaona vifaa vyote vitakavyo tumika katika hilo jengo lake beside his office lazima vitatoka njee bila kulipia ushuru.
 
Back
Top Bottom