Changamoto kwenye muswada wa Bima ya Afya kwa wote

Changamoto kwenye muswada wa Bima ya Afya kwa wote

Kba

Member
Joined
Jul 15, 2022
Posts
5
Reaction score
5
Mimi kama Mtanzania ninayeishi kijijini kwanza naipongeza serikali kuja na MUSWADA wa Bima ya Afya kwa watu wote ni Jambo jema ktk kunusuru afya za watu wake. Changamoto ninayoiona hapa ni hizi gharama za kila mwanachi mwenye familia ya watu sita kuchangia 340,000. Huu ni mzigo mkubwa na ni adhabu kwa wananchi endapo huu mswada utapitishwa na kuwa Sheria itakulazimu ili upate BIMA ya afya, utalipia hiyo pesa 340,000 na 84,000 kwa mtu asiye na familia

Sasa hivi gharama za maisha zipo juu hasa kwa sisi wanyonge ni ngumu kulipa hiyo pesa kulinganisha na hali ya sasa, wapo watakaoweza kumudu hiyo gharama Ila wengi hawatamudu na huo ndo ukweli. Kama mwananchi anashindwa kumudu gharama za kununua debe la mahindi karibia elfu 30, leo ataweza kutoa hiyo 340,000 Tena kwa lazima?

CHANGAMOTO nyingine tayari Kuna watu wanazo BIMA Ila huduma anayopata akienda hospitali ni mbovu anaweza ambiwa aende akanunue dawa nje ya hospitali na BIMA anayo hii pia inavunja moyo watu kufuatilia BIMA.

USHAURI wangu kwa mamlaka husika watoe ruzuku au waweke kodi kwenye bidhaa kama vile bia, sigara nk ili kuchangia kwa wale wananchi ambao hawataweza kulipa hiyo gharama.

Tofauti na hapo hili nalo ni bomu ambalo litakuja kuitesa Serikali baadaye.
 
Mkiwa watu wawili unalipa ngapi?kama sita ni laki 3 na kitu
 
Back
Top Bottom