Kutokana na changamoto ya mafuta kubwa bei juu nashauri chukua hii gari.
Ukiweza chukua Fit hybrid 2013 au 14 aiseee utakuwa huru sana na utapenda hizo gari.
Hizi gari kwanza zina space kubwa sana ndani yake na kwenye buti la mizigo. Unaliinjoi ukiendesha. Unaweza kukaa nalo hata miaka 5 we ni kumwaga oil tu . Hizi gari hazina magonjwa kabisa, zinamudu mazingira magumu na zinazidi kwa mbali sana gari za type zake kama IST, Sienta, Vitz, Ractis etc.
Fit ya kawaida inaenda km 13 hadi 15 kwa lita wakati hybrid inaenda hadi km 30.
Changamoto ya hizi gari ni kama ifuatavyo
1. AC yake haina nguvu
2. Haina tairi la akiba, kuna motor/pum ndani ya kujazia hewa na oko yake
3. Ipi chini sana kwa hiyo ukipakiza abiria ukapita rough road inazingua.
4. Usiendeshe spidi kubwa zaidi ya 120 zinahama