Changamoto na ushauri wa gari aina ya Honda Fit GE6 ya mwaka 2009

Changamoto na ushauri wa gari aina ya Honda Fit GE6 ya mwaka 2009

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
1,644
Reaction score
1,648
Watu wa Mungu habari!
Naomba kujua toka kwa mwenye uzoefu wa kutumia hii gari aina ya Honda Fit GE6.

Ina changamoto gani, ina ubora gani na bei yake hapa Tanzania, upatikanaji wa spare zake n.k

Natamani sana kumiliki hili gari!

Ahsante
CMmglCJzrVIym0uK_1.jpg
j4q585DUamG9zaa4_8.jpg
 
Kutokana na changamoto ya mafuta kubwa bei juu nashauri chukua hii gari.

Ukiweza chukua Fit hybrid 2013 au 14 aiseee utakuwa huru sana na utapenda hizo gari.

Hizi gari kwanza zina space kubwa sana ndani yake na kwenye buti la mizigo. Unaliinjoi ukiendesha. Unaweza kukaa nalo hata miaka 5 we ni kumwaga oil tu . Hizi gari hazina magonjwa kabisa, zinamudu mazingira magumu na zinazidi kwa mbali sana gari za type zake kama IST, Sienta, Vitz, Ractis etc.

Fit ya kawaida inaenda km 13 hadi 15 kwa lita wakati hybrid inaenda hadi km 30.

Changamoto ya hizi gari ni kama ifuatavyo
1. AC yake haina nguvu
2. Haina tairi la akiba, kuna motor/pum ndani ya kujazia hewa na oko yake
3. Ipi chini sana kwa hiyo ukipakiza abiria ukapita rough road inazingua.
4. Usiendeshe spidi kubwa zaidi ya 120 zinahama
 
Back
Top Bottom