Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,958
OKTOBA 22, 2019
KUTOKEA SAME MKOANI KILIMANJARO.
Kukosekana wodi ya wajawazito katika zahanati ya Lugulu iliyopo Wilaya ya Same, kumesababisha wanaotaka kujifungua watumie chumba kimoja na wagonjwa wanaosafishwa vidonda.
Wakizungumza na Mwananchi, wakazi wa Kijiji cha Lugulu ilipo zahanati hiyo wamedai kuwa baada ya kujifungua wanawake walikuwa wakibebeshwa uchafu kutokana na kukosekana shimo maalumu la kutupia taka hizo.
Jerna Basili, mkazi wa kijiji hicho alisema kitendo cha wao kuchanganywa chumba kimoja na wagonjwa wengine ni udhalilishaji usiovumilika.
“Hebu fikiria mama anajifungua sehemu ambayo kuna wagonjwa wengine wanasafishwa vidonda. Licha ya kumdhalilisha mama, pia tunamuweka katika mazingira hatarishi mtoto anayezaliwa,” alisema.
Jerna alisema awali wanawake hao walikuwa wakibebeshwa uchafu, lakini hivi karibuni uongozi wa zahanati hiyo umeamuru uchafu huo utupwe chooni.
“Hebu fikiria lile kondo linatupwa kwenye choo cha shimo, hicho choo kitaingilika kweli kama vinachanganyika huko, na usalama wa afya kwa watumiaji wengine ukoje?” Alihoji Jerna.
Waziri Mhusika!