milionea wa kesho
JF-Expert Member
- Dec 28, 2015
- 328
- 631
biashara yako ipo mtaa gani? Nenda sokoni nunua futari ndizi mbivu mshale, magimbi, tambi, mihogo, kama unajua pika kalimati, ndizi mbichi utumbo, nunua tende kidogo, pika na uji mwepesi usiwe mzito sana (vyakula vikolee nazi). Weka bango KARIBUNI KWA FUTARI, hakikisha uji unakuwa free (wape offer wanaofunga kuonyesha unawajali sana) toa viti kidogo na tandika mikeka safi unaetaka anakaa, Utawapata hata wasio funga, hakikisha mboga smaki ama nyama unaweka ya kutosha, panga bei zako vizuri kisha mwezi ukiisha lete mrejesho hapa.
asante sana mkuu...tatizo mgahawa wangu upo maeneo ya sokoni ambapo basically watu wanakuepo mchana na asubuhi tu
As far as unapika chakula kizuri watakufata hata wa majumbani na ma hotpot yao.
Fuata ushauri wa jamaa.asante sana mkuu...tatizo mgahawa wangu upo maeneo ya sokoni ambapo basically watu wanakuepo mchana na asubuhi tu
Fuata ushauri wa jamaa.
Uzur wa futari inauzika hata barabarani kwa sababu muda wa kufuturu jua linakuwa limezama.
Kama unahisi hapo sokoni pamejificha sana kiasi Cha kutoonekana hamisha mabenchi yako na viti kaweke kandokando ya barabara wanakopita abiria/wasafiri au hata wanapopita wafanyakazi wa aina yoyote watakufuata.
Hapo kwenye mgahawa wako bandika tangazo tu kwamba umehamia mtaa fulani kwa sababu ya kuuza futari.
Ni kweli hakuna dawa zaidi ya utamu wa chakula.Mkuu mbu wa dengue uzuri wa futari hizi huwa ni za msimu, ukichanganya na vitu kama maharage ya sukari, njugu mawe na bidhaa kama hizo na watu wakishagundua utauza tu.