biashara yako ipo mtaa gani? Nenda sokoni nunua futari ndizi mbivu mshale, magimbi, tambi, mihogo, kama unajua pika kalimati, ndizi mbichi utumbo, nunua tende kidogo, pika na uji mwepesi usiwe mzito sana (vyakula vikolee nazi). Weka bango KARIBUNI KWA FUTARI, hakikisha uji unakuwa free (wape offer wanaofunga kuonyesha unawajali sana) toa viti kidogo na tandika mikeka safi unaetaka anakaa, Utawapata hata wasio funga, hakikisha mboga smaki ama nyama unaweka ya kutosha, panga bei zako vizuri kisha mwezi ukiisha lete mrejesho hapa.