Changamoto ya choo kupata kutu

plumber hydrogen

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2022
Posts
881
Reaction score
1,537
Habari zenu ndugu zangu wa JF..Leo tuangalie sababu zinazo pelekea choo kupata pindi tu kinapo anza kutumiaka

1.Kununua choo kilicho na ubora mdogo hapa ata ukifanyie usafi vipi choo lazima kishike kutu na kubabdilika rangi unapo fanya maamuzi ya kununua choo hakikisha umenunua choo imara kuepukana na kadhia hiyo..

2.Kutumia kemikali kali kuna baadhi ya watu utumia choo kufulia,kuogea au kufanya matumizi mengine nje ya yale ya kawaida..Kemikali kama jiki n.k uondoa ubora wa choo kwa kwa kiasi flani..

3.Kuto fanya usafi mara kwa mara japo hii sio sababu kubwa endapo choo kina ubora ila kama hakina ubora fanya usafi mara kwa mara...

NB Weka mazingira ya choo safi kwa mda wote kuepuka magonjwa...
 
Mwaga thick bleach uache kama dakika kumi ndiyo usafishe kwa brush ya choo. Sakafu safisha na maji yaliyochanganywa na bleach. Tumia ndoo na dekio la mti kwa afya yako mwenyewe.

Ukikosa bleach majivu yanafanya kazi vizuri pia au becabonate soda ile ya kuokea mikate.
 
Sasa Mbona ujaeleza kuhusu hizo Marumaru Maana hapo hakuna choo kisafi katika picha
 
choo ama sink, unanunua choo
Kitaalam sink ni kitu kingine sink ni kama slope sink,kitchen sink na kitaalam choo tunaita (water closet) choo kazi yake ni kupokea uchafu wa ndani ya mwili kinyesi ,mkojo na sink kazi yake kupokea uchafu nje ya mwili hapa ni kama kunawa kuoga kufulia kuosha vyombo kuosha mboga mboga n.k..So choo na sink ni vitu viwili tofauti...
 
Kweli kabisa
 
Hiyo siyo kutu. Ni mchanganyiko wa uchafu, mold na soap scum.
 
Hiyo bleach inapatikana wapi
 
Kwenye minmarket zetu aina gani ya bleach inafaa??
 
Mwalimu wetu wa sayansi kimu (RIP) alikua anatuambia choo cha mstaarabu ukiingia unaweza kupewa chakula na ukala humo lakini choo cha asiye staarabika hata kujisaidia unawaza utamaliza saa ngapi.
 
Sada coca-cola ni dawa tosha, mwangia uone majibu na utashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…