Changamoto ya kupotea kwa mimba

Changamoto ya kupotea kwa mimba

SinaJambo

New Member
Joined
Jan 4, 2025
Posts
1
Reaction score
1
Poleni na majukumu wadau wa afya. Nina changamoto moja ambayo inamsumbua mke wangu kwa kipindi cha miezi mitatu sasa.
Ana dalili zote za mimba ambayo haikui na tukipima hospitali vipimo vinaonyesha ana mimba lakini nasikitika nnapoona mimba ya mke wangu inapotea. Naombeni msaada wa mawazo. Napokea mawazo ya aina zote hata upande wa pili, nahofia asije kuwa kakanyaga vitu vibaya.
 
Pole sana!

Sijaelewa mkeo amepoteza mimba ngapi?
Na kama mimba zaidi ya moja zimepotea je zinapotea ikiwa na miezi mingapi?

Je una maanisha kwamba mimba zinatoka au vipi?

Hujatuambia kama mna watoto wangapi au ndiyo mmeanza maisha ya ndoa?

Naomba uelezee vizuri jinsi matatizo hayo yanavyotokea kwake ili tuelewe vyema tuweze kukushauri.
 
Habari,

Kipimo cha mimba cha mkojo,kina pima uwepo wa homoni moja inayozalishwa na kondo la nyuma la mtoto mimba inapotungwa. Lakini homoni hii huweza kutengenezwa mwilini kwa sababu zingine zisizohusiana na mimba, ama ikaendelea kuonekana kwenye mkojo hata baada ya mimba kuharibika.

Kipimo cha uhakika kama mtu ni mjamzito ni picha ya Ultrasound, hiyo ikisema mimba ipo, unakuwa na uhakika ni kweli ipo. Na pia,inaweza kuonyesha mtoto kama yuko hai (akifariki tumboni, ataonekana hakui japokuwa miezi inaenda)

Jaribu kupima picha ya tumbo la uzazi, Ultrasound.
 
Dalili unazosema ni kama mimba imetunga nje ya kizazi (Ectopic Pregnancy) na kwa kesi anatakiwa kufanyiwa operation nenda hospital na uonane na daktar wa wanawake.

Ukizidi kuchelewa kupata matibabu inaweza kuhatarisha afya ya mke wako.
 
Back
Top Bottom